Dodoma: Hakuna cha Mayele kutetema

Saturday May 14 2022
dodoma pic
By Ramadhan Hassan

Dodoma. Kocha Msaidizi wa Kikosi cha Dodoma Jiji Mohammed Muya amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga huku akidai wamejipanga kuhakikisha mshambuliji wa Yanga Fiston Mayele hatetemi.

Dodoma Jiji inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa Ligi kuu ikiwa na alama 28 huku vinara Yanga wakiwa kileleni na pointi 57.

Kocha huyo amesema:  “Hiyo kutetema kwetu hatuifikirii  kabisa nimekwambia  sisi niwahitaji   kutetema hakupo kesho,”

Amesema morali ya wachezaji ipo juu na michezo yao mitatu ya mwisho wamepata alama saba  wakishinda dhidi ya  Biashara, Mbeya City na kutoka suluhu dhidi ya Polisi Tanzania ugenini.

“Kama mwalimu unajua kinachotakiwa kwa wachezaji wako hakuna cha kuogopa timu yoyote, vigezo vya kuwa washindani tunavyo tunawaita mashabiki wetu waje.

Mchezaji wa timu hiyo,Omary Kanyoro amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo amewaomba  mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Advertisement
Advertisement