Coastal Union waivutia kasi Simba

Muktasari:

MATOKEO yasiyoridhisha ya Coastal Union yamewaumiza wachezaji wa timu hiyo na wameapa kuisimamisha Simba, Mei 11, timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

MATOKEO yasiyoridhisha ya Coastal Union yamewaumiza wachezaji wa timu hiyo na wameapa kuisimamisha Simba, Mei 11, timu hizo zitakapokutana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Coastal Union bado inawaza kipigo cha mabao 7-0 ilichopewa na Simba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara uliofanyika Novemba 21, mwaka jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Beki wa Coastal Union, Hans Masoud alisema yeye na wachezaji wenzake wanatambua umuhimu wa kupata pointi tatu katika mechi hiyo, hivyo watahakikisha wanacheza kwa juhudi ili kukamilisha jambo lao.

“Tunatambua kwamba Simba ina kikosi kizuri, lakini sisi kama Coastal Union tunahitaji ushindi katika mechi hiyo kuliko kitu kingine,” alisema Masoud.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Coastal Union, Omar Mwambashi alisema tayari mikakati imeshawekwa kuhakikisha kila mechi ijayo inachezwa kwa umakini ili kuinusuru timu kushuka daraja.