Casillas huyoo Burundi

Friday August 05 2022
Casillas PIC
By Thomas Ng'itu

KIPA Hussein Sharifu 'Casillas' amejiunga na klabu ya Inter Star inayoshiriki Ligi Kuu nchini Burundi.

Casillas amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo akiwa mchezaji huru kwa muda mrefu baada ya kutojihusisha kabisa na mpira wa miguu nchini.

Mdogo wa Casillas, Fahad Abdallah amesema kaka yake amesaini mkataba na timu hiyo baada ya kuafikiana.

"Casillas amesaini Burundi kule na tayari ameanza maandalizi ya msimu mpya,"amesema kwa kifupi.

Alipotafutwa Casillas amesema ni jambo zuri kwake kusaini timu ya nje ya nchi baada ya kujiweka pembeni kwa muda.

"Namshukuru Mungu baada ya kukaa nje ya uwanja nimerudi uwanjani, nimeamua kuja huku kwa sababu ya kubadilisha mazingira, nyumbani kunalemaza."

Advertisement

Casillas amewahi kutamba na timu za Coastal Union, Simba, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.

Advertisement