Bwalya atambulishwa rasmi Amazulu

Thursday June 23 2022
bwalya pic
By Leonard Musikula

ALIYEKUWA Kiungo mshambuliaji wa Simba, Rally Bwalya ametambulishwa ramsi leo Juni 23 na klabu yake mpya ya Amazulu Fc ya nchini Afrika Kusini.

Bwalya anaungana na wachezaji wengine 10 waliosajiliwa na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni sehemu ya uboreshaji wa kikosi chao cha msimu ujao akiwemo beki Thendo Mukumela (24) akitokea Cape Town Spurs, Veluyeke Zulu (27) anayetokea na Riaan Hanamub (27) wote wakitolea Chippa United

Wengine ni Winga Dumisani Zuma (27) anayetoka Kaizer Chiefs, Mnigeria Augustine Kwem (24) akitokea TS Galaxy pamoja na Mmalawi Gabadinho Mhango (29) anayetokea Orlando Pirates.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo sasa amesalia na mmoja huku ikidaiwa amesaini miaka miwili na Amazulu hivyo atacheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Advertisement