Bushoke: Simba itakutana na sapraizi kwa Mkapa

Monday May 03 2021
mastaa pic1
By Clezencia Tryphone

MSANII mkongwe wa bongo fleva, alimarufu kama Bushoke amesema Yanga inaweza ikaisapraizi Simba kwenye mechi ya dabi, itakayopigwa Mei 8, mwaka 2021 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Bushoke ameliambia Mwanaspoti online, leo Jumatatu ya Mei 3 kwamba kwa namna Yanga ambavyo ilionekana ina muenendo wa kupanda na kushuka, Simba inaweza ikaja kichwakichwa na kuambulia maumivu ambayo hawakuyatarajia.

Bushoke ambaye ni shabiki wa Yanga kindakindaki amesema mechi ya dabi haina mwenyewe hata kama timu moja inakuwa kwenye bora mwamuzi anakuwa ni dakika 90.

"Ni kweli Yanga ilianza vyema lakini baadae ni kama ilianza kuondoka kwenye laini na kuipisha Simba kileleni, lakini hilo halimanishi kwamba Simba inaweza ikaifunga Yanga na ndio maana ni mabingwa wa kihistoria," amesema na ameongeza kuwa;

"Simba haijawahi kuwa wajanja mbele ya Yanga, kwanza wao ndio wana presha na mchezo huo, sasa kelele na tambo zote dakika 90 ndizo zitakazoamua nani mtani wa mwenzake,"amesema.

Advertisement