Bure kuiangalia Twiga kwa Mkapa

Wednesday October 20 2021
bure pic
By Mustafa Mtupa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)  limetoa taarifa ya kuruhusiwa kwa mashabiki katika mchezo  wa kufuzu michuano ya Afcon kati ya Twiga Stars na Namibia utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.
Katika taarifa hiyo TFF ilifafanua kwamba wapokea ruhusa hiyo ya kuingiza mshabiki kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) saa 7:25 mchana.
Aidha kutokana na muda mfupi uliopo hadi kufikia mchezo huo kuanza saa 10:00 TFF wameruhusu mashabiki  kuingia bure.
Baada ya mchezo huo Twiga itakuwa na kibarua cha mchezo wa marudiano kule Namibia Oktoba 23 na ikifanikiwa kupita itakutana na mshindi kati ya Malawi na Zambia.

Advertisement