Barbara: Kazi ndio imeanza Simba

Tuesday February 23 2021
brabra pic
By Ramadhan Elias
By Olipa Assa

MTENDAJI mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amefurahishwa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly na kusema unawapa nguvu ya kuendelea kupambana zaidi.

Barbara amesema ushindi huo ni faraja kwa Simba kuhakikisha wanapiga hatua kubwa zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya ushindi huo, Simba ina pointi sita na mabao mawili, baada ya kushinda mechi ya kwanza na As Vita.
Jambo ambalo Barbara ameliona limewaweka katika ari ya morali na wachezaji wao kujiamini zaidi.
"Vijana wetu wamepambana kuhakikisha wanaliwakilisha vyema  Taifa la Tanzania kuonyesha soka letu nilaushindani na tumeamua kupambana," amesema na ameongeza kuwa;
"Kazi ndio imeanza mashabiki waendelee kuishangilia timu yao, ili mwaka huu tufanye vitu vyakushangaza," amesema.


MASHABIKI WAMPA SALUTI BARBARA
Wakati Barbara anatoka kwenda kupanda gari yake, alisindikizwa na msafara wa wanaume wasiopungua 10 huku akipita katikati yao.
Baada ya kuona hivyo mashabiki walianza kumshangilia na kumuita ni mwanamke wa shoka.

Mwanaspoti limewashuhudia wakimwambia "Barbara heshima yako wewe ni zaidi ya mtu mmoja, unafanya makubwa tunakuombea,".

Advertisement
Advertisement