Yanga yashusha mtaalam kutoka Raja Casablanca

Thursday April 22 2021
raja pic
By Thomas Ng'itu

MABOSI wa Yanga wanamshusha kocha wa viungo Jawadi Sabri kutoka nchini Morocco.

Sabri amekuja kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa viungo wa timu hiyo, Edem Mortits ambaye aliondoka siku chache baada ya bosi wake Cedrick Kaze kutimuliwa.

Kocha huyo ametua leo jioni na moja kwa moja atasaini mkataba. Ana rekodi ya kufanya vizuri akiwa na Raja Casablanca iliyochukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini Morocco msimu wa 2019-2020.

Pia kocha huyo alikuwa na kikosi hicho na kufika hatua ya nusu fainali katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita dhidi ya Zamalek.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa, ulisema; “Makocha wote ambao wapo na Nabi ni watu ambao alishawahi kufanya nao kazi awali.”

Advertisement