#WC2018: Cheki kocha Antonio Pizzi

Muktasari:
Mnamo Januari 26, 2016 alichukua mikoba ya Jorge Sampaoli ya kuifundisha Chile, ambapo aliiwezesha timu hiyo kubeba ubingwa wa Copa America huko Marekani.
Ni kocha mzoefu na mchezaji wa zamani wa Argentina.
Mnamo Januari 26, 2016 alichukua mikoba ya Jorge Sampaoli ya kuifundisha Chile, ambapo aliiwezesha timu hiyo kubeba ubingwa wa Copa America huko Marekani.
Pizzi pia aliweza kuipeleka Chile katika hatua ya fainali ya kombe la mabara na kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani 2017.
Licha ya mafanikio hayo, lakini Chile ilishindwa kufuzu katika kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2018.
Novemba 2017, aliichukua Saudi Arabia, hivyo anategemewa kufanya makubwa kwenye fainali hizo baada ya kuzikosa mara mbili mfululizo.