Ufaza kumponza Niyonzima

Ufaza kumponza Niyonzima

IPO minong’ono kuwa Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima anajifanya ‘faza’ kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Cedrick Kaze kitu ambacho kinaweza kuathiri kiwango chake kama asipokuwa makini.

Kwa namna ambavyo inaonekana ni kama Niyonzima amelizika na haonyeshi kuwa na njaa za kuipigania nambari nane ambayo alivyokuwa na badala yake taratibu ameanza kusahaulika kikosini.

Ni Feisal Salum na Mukoko Tonombe ambao kwa sasa wamekuwa tegemezi kwenye kikosi hicho kwenye eneo la kiungo na inapobidi mmoja wapo asipokuwa kwenye kiwango bora, hubidi Kaze kumtumia Zawadi Mauya kitu ambacho kimezua mijadala huko vijiweni. Wazee wa vijiwe kwa busara zao wanasema inawezekana kuwa Niyonzima itakuwa najifanya ‘faza’ akiwa na maana ya kuwa yeye ndiye yeye kitu ambacho pengine havutiwi naye kocha wake na kuendelea na maisha mengine bila kiungo huyo fundi raia wa Rwanda.