Tshabalala: Tulieni muone kwa Orlando

Tshabalala: Tulieni muone kwa Orlando

NAHODHA msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amewatuliza mashabiki na kuwasisitiza kwamba wanajua wanachopaswa kufanya Jumapili dhidi ya Orlando Pirates.

Tshabalala amekuwa akiiongoza Simba katika michuano hiyo ya CAF kutokana na nahodha mkuu, John Bocco kuwa majeruhi amewatoa hofu ma-shabiki juu ya uwezo wao mbele ya Pirates akisema; “Tulieni muone, hawa wetu tunawapiga. Tunajua wapinzani

wetu ni timu bora, ila naamini sisi ni bora pia ma tumejipanga vizuri kupata matokeo chanya. Kila mchezaji anajua umuhimu wa mechi hii, tunacheza nyumbani hivyo tunahitaji ushindi ili kurahisisha kazi katika harakati zetu za kutinga nusu fainali na tupo tayari kupambana ili kufanikisha hilo,” alisema Tshabalala.

“Mashabiki zetu tunawakubali, wao ndio wanatupa nguvu kubwa ya kufanya vizuri uwanjani nawaomba wajitokeze kwa wingi kutusapoti na sisi hatutawaangusha.”

Mwanaspoti linajua Simba imekamilisha mipango yote kuelekea mechi hiyo na Jumatatu kocha mkuu wa klabu hiyo, Pablo Franco alikuwa na kikao kizito na Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na kumuahidi Ushindi.

Katika mechi hiyo itakayopigwa April 17 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba inahitaji ushindi ili kutanguliza mguu nusu fainali kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa Aprili 24, Afrika Kusini.