Nyota Simba, Yanga wakwama

NYOTA wa zamani wa Simba na Yanga akiwamo, George Masatu, Mustapha Hoza, Dua Saidi, Edibilily Lunyamila, Salvatory Edward, Bakari Malima, Akida Makunda, Haruna Moshi, Idd Moshi, Saidi Swedi, Tumba Swedi na Obeid (Clement) Kahabuka wamekwaa kisiki kwa kushindwa kuzipa ubingwa timu walizozichezea kwenye bonanza la kufungua msimu mpya wa soka barani Ulaya.

Katika bonanza hilo lenye kauli mbiu ya biriani iendelee lililoandaliwa na DStv, nyota hao waliounda timu wanazoshabikia Ulaya za Arsenal, Liverpool na Manchester United walikwaa kisiki mbele ya timu ya Wanahabari za Michezo, Taswa SC iliyotwaa ubingwa juzi kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Taswa ilitwaa ubingwa huo kwa kuifunga timu ya mashabiki wa Arsenal mabao 3-0, kabla ya kuwachapa Mashabiki wa Manchester United 1-0 na kisha wale wa Liverpool bao 1-0.

Makunda na Hoza waliiongoza Arsenal, Masatu, Zubery Katwila, Malima na Jerson Tegete wao walikuwa ‘team’ Manchester na Kahabuka, Salvatory na Lunyamila walikuwa ‘team’ Liverpool ambayo ilitwaa ushindi wa pili ikiwa chini ya nahodha Lubigisa Madata.

Mkuu wa Masoko wa DStv Tanzania, Ronald Shelukindo alisema wana mkakati bonanza hilo lifanyike kila mwaka kwenye mikoa tofauti.

“Wanamichezo wa zamani hawakupata nafasi ya kuonekana kwani wakati wao mitandao ya kijamii, hata televisheni havikuewpo kama hivi sasa, hivyo tnpowakutaisha hivi hata kizzi cha sasa kinapata kuwafahamu,” alisema Shulikindo huko Hoza naye licha ya timu yake ya Arsenal kukosa ubingwa, alisema asili ya mpira birian ni kwenye timu hiyo.

“Pira Birian ni asili ya The Gunners, hilo halina ubishi ilianza na Mzee Arsene Wenger mpaka sasa, hivyo kama mmoja wa mashabiki wao, msimu ujao pira biriani linaendelea,” alisema Hoza, beki wa zamani wa Simba.