Nabi: tukutane Dar, Senzo aja na mbinu mpya

Nabi ashtukia mastaa Yanga

KOCHA wa Yanga Nesreddine Nabi ameshtuka kusikia timu yake imetupwa nje ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi lakini akasisitiza sasa wanakoki silaha zao upya na watarejea uwanjani kwa nguvu kubwa zaidi.
Nabi ambaye hakuwa sehemu ya kikosi hicho kwenye mashindano hayo wakitema taji hilo, ameliambia Mwanaspoti kutoka Ubelgiji wachezaji wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na kujua sasa ni vita na watapaswa kupambana kwa nguvu zaidi kurejesha imani kwa mashabiki na utamu waliouzoea.
“Sikuwa na wasiwasi tungeishia nusu fainali, nimeshtuka, namwamini Kaze (Cedric) na hata wachezaji lakini hatua tuliyofikia chochote kinaweza kutokea, penalti ni kama kamari,” alisema Nabi.
Hata hivyo, Nabi alisema matokeo hayo yanawakumbusha wanatakiwa kurudi kwenye ligi wakiwa na akili mpya itakayorudisha heshima yao kwa mashabiki wao ambao hawatakuwa wamefurahishwa kutolewa kwao.
Alisema wanatakiwa kurudisha ushindi katika timu yao kwa kushinda ligi na lile la Azam Shirikisho litawafuta machozi mashabiki wao.
“Mashabiki hawawezi kuwa na furaha timu inapofungwa lakini bado wanatakiwa kuwa pamoja na timu yao, ni vizuri tukipoteza pamoja  na tukishinda pamoja.
“Nitawaambia wachezaji na timu kwa jumla lazima sasa turudi na nguvu katika ligi, tunatakiwa kurudisha ubora wetu ambao umetufanya mashabiki kuwa na sisi na kutuamini kama timu, tukishinda mataji tutawafurahisha. Hili limeshapita sasa,” alisema.

Senzo akazia
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa ameunga mkono kauli ya Nabi akisema ni wakati wa mashabiki wao kuamka na kurudi katika mapambano ya kusaka ubingwa.
“Hakuna anayefurahia matokeo haya, Kombe la Mapinduzi lilikuwa ni moja