Morrison, Tshishimbi ndio mifano ya ‘fighting spirit’

KWA sasa hakuna mechi zinazochezwa kwa sababu ya janga la corona na ndicho kipindi ambacho baadhi ya klabu zinatumia kuasses vikosi vyao kusubiri kipindi cha usajili.

Katika ‘sports management’ kuna mambo manne ambayo huwa yanatakiwa kufanywa na uongozi baada ya kufanya ‘assessment’ ambayo ni Planning, Organization Directing na Staffing.

Katika Staffing hapa uongozi hujikita kuangalia ‘human resorces’ au rasilimali watu ambao wapo katika taasisi au kampuni fulani ili kuona kama inahitajika kuongeza au kupunguza watu.

Klabu nyingi huwa zinaanzia katika kipengele cha nne na Yanga tunaweza kusema nao wameanzia hapo kwa kuweza kuwabakisha nahodha wao Papy Tshishimbi na mshambuliaji Bernard Morrison.

Hakuna asiyejua uwepo wa Tshishimbi umekuwa na mchango gani kwa Yanga na kumfanya awe mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo hiyo.

Tangu alipoingia akitokea katika timu ya Mbabane Swallows ya eSwatini amekuwa kwenye kiwango bora cha jumla ukiondoa hali ya kawaida ya mchezaji kutokuwa vizuri katika mechi mojamoja.

Amekuwa mhimili mkubwa muda wote katika eneo la kiungo na kuwa msaada mkubwa kwa timu katika mechi mbalimbali ambazo imekuwa ikicheza tangu alipojiunga nayo.

Amekuja kutumikia Yanga kama kiungo mkabaji muda wote kutokana na uwezo wake wa kupokonya mipira, energy aliyonayo, kuilinda timu na kuziba mianya ya wapinzani eneo la katikati.

Wakati mwingine amekuwa akitumika katika nafasi tofauti tofauti kama vile kiungo mshambuliaji, mshambuliaji wa pili na hata beki kulingana na mahitaji ya mchezo husika kwa wakati huo.

Kitaalam wachezaji wa aina ya Tshishimbi tunaita versatile players. Ni mchezaji anayejitolea na kucheza kwa kujituma muda wote anapokuwa uwanjani na huwa hakati tamaa.

Ni mchezaji ambaye amekuwa dynamic na kumbakiza yeye watakuwa wamemaintain hayo. Watakuwa wamefanya jambo jema.

Kabla ya usajili, lazima viongozi wafanye evaluation. Pre evaluation na post evaluation. Walipomsajili akitokea Mbabane Swallows, walifanya ‘pre evaluation’ na sasa wamefanya ‘post evaluation’ wakaona wahakikishe wanapambana hadi wakambakiza.

Kumbakisha Tshishimbi limekuwa ni jambo la maana na lenye msaada mkubwa kwa Yanga ambayo sasa ipo katika mipango ya kutengeneza timu bora na yenye ushindani.

Kuhusu Bernard Morrison nadhani kila Mtanzania anafahamu kuhusu uwezo wake tangu alipoanza kuichezea Yanga.

Morrison ni mchezaji ambaye anajiamini, anajua nini anachokifanya ndani ya uwanja na mwenye uamuzi wa haraka anapokuwa na mpira.

Ana uwezo wa kucheza yeye kama yeye. Kuchezesha timu na wenzake. Faida ya tatu ni kufunga na kupiga pasi za mwisho kwa wenzake.

Wachezaji aliowakuta wengi wao hawakuwa na kiwango kama chake. Hivyo akawa anajikuta anatumia nguvu nyingi na maarifa mengi.

Angekuwa miongoni mwa wafungaji ambao wangekuwa wanaongoza kwa kufunga idadi kubwa ya mabao.

Moja wangekosa wachezaji muhimu. Duniani katika timu zozote zile hasa ile iliyo na malengo ya kutwaa ubingwa kunakuwa na wachezaji wa aina tatu.

Moja ni mchezaji wa kawaida ordinary players. Kundi la pili ni key players na kundi la tatu ni senior players. Tshishimbi yupo katika kundi la tatu. Ni mchezaji muhimu lakini amedumu kwa muda mrefu.

Katika mechi ambayo ni ngumu na muhimu (crucial) key players na senior players ndio mara nyingi huwa wanapangwa.

Yanga kuwapoteza hao ingekuwa imepoteza faida na vitu vingi. Wangekuwa wameondoka maana yake criteria zote za ufundi na mbinu wangekuwa wamezipoteza.

Kumuacha Tshishimbi ingekuwa ni uzembe kwa sababu ni mchezaji muhimu na mkongwe na Morrison ni mchezaji ambaye ndani ya muda mfupi ameonyesha kitu.

Lakini upande mwingine hao ni wachezaji ambao behaviours zao zimekuwa ni za kuwa mfano wa kuigwa na wachezaji wadogo na wale wanaoingia katika klabu ambao wanawatazama kama ‘role models’ wao.

Hao wachezaji wawili wana ‘fighting spirit’ na ‘commitment’ ya hali ya juu.