Kama zali Lamine Moro kurejesha majeshi Bongo

Monday June 20 2022
Lamine PIC

KAMA mipango itaenda ilivyopangwa basi kuna uwezekano mkubwa kwa beki wa zamani wa Simba na Yanga, Lamine Moro akarejea nchini kucheza katika Ligi Kuu Bara.

Lamine anayekipiga kwa sasa katika timu ya Newroz SC ya Iraq, aliyojiunga nayo Januari mwaka huu baada ya kutoka Yanga msimu uliopita sasa ameingia kwenye rada za klabu ya Azam FC.

Habari kutoka ndani ya Azam zinasema kuwa, Lamine aliyeachana na Yanga msimu uliopita na kujiunga AS Kigali ya Rwanda kabla ya kutimkia Iraq anasakwa ili kuja kucheza beki ya kati kutokana na pengo la Yakubu Mohamed na kujiangaa kuondoka kwa mkongwe Aggrey Morris.

Awali ilidaiwa, Yakubu alikuwa arejeshwe na alikuja nchini hivi karibuni kuzungumza na mabosi wa Azam, lakini mipango kama inaenda sivyo hivyo chaguo lilifuata likawa kwa Lamine aliyewahi kucheza Simba kwa muda mfupi.

Advertisement