Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amejitokeza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye Siku ya Mwananchi na kutambulisha kikosi cha mwaka 2022/23.
“Mimi sijihusishi na masuala ya michezo hapa nimelipwa tu kama MC wa kujitegemea. Yaani mimi ni MC wa mtaani tu tena nikimaliza hapa naenda na mambo yangu”. amesema Manara
Manara amefungiwa kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili na faina ya Sh20 milioni alikuwa mshereshaji katika shughuli hiyo.