UCHAMBUZI: Namungo siwadai wamenilipa zaidi ya deni ninalowadai

Simba anatishia kila anayekuja mbele yake kwa jinsi alivyokua mtamu wa kujua kutafuta ushindi.

Simba imekuwa na kiwango bora zaidi msimu huu wakishinda mechi zao nyingi na sasa wanasubiria kujua wanakutana na nani katika hatua ya robo fainali na naamini katika kusubiri huko ratiba zipo timu ambazo zinaweza kukutana na wekundu hao zikawa na hofu.

Upande mwingine wa Kombe la Shirikisho Afrika kuna Namungo ya Lindi ambayo nayo ipo katika hatua ya makundi lakini huko hawa ndugu zetu hawako sawa sana kuna mshtuko wanaupata wa ukuaji.

Namungo mpaka sasa haijashinda mchezo wowote katika hatua hiyo ya makundi na inashika mkia hii sio nzuri kwao lakini kuna kitu wanajifunza.

Binafsi hata Namungo afungwe 10 sitajutia nab ado nitawatambua kama mashujaa ambao wamefikia malengo yao makubwa na katika hili nitawatetea vyema kwa hiki ambacho wamefanya jamaa hawa kutoka Lindi pale Ruangwa.

Namungo huu ni msimu wao wa pili katika ligi kuu Tanzania Bara na msimu wao wa kwanza tu wakafanikiwa kupata nafasi ya kucheza mashindano ya Afrika wakishika nafasi ya pili kupitia mashindano ya Kombe la FA Azam Shirikisho wkaifungwa nan a Simba ambao sasa wanawatoa jasho Al Ahly.

Kukata tiketi huko kwa Namungo msimu huu wa kwanza kwao katika mashindano ya Afrika wanapambana kwa jasho mpaka wanatinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Huko hatua ya Makundi maisha yalivyokosa huruma wakakumbana na bahati mbaya wakipangwa kundi moja na Pyramids ya Misri klabu tajiri sana hii inayosumbua ligi ya Misri lakini pia wakapangwa na Nkana ya Zambia ambayo ina uzoefu mkubwa katika mashindano haya na kama haitoshi wakapangwa na vigogo vigogo wengine wa Kiarabau Raja Casablanca ya Morocco.

Ukiziangalia kwa upana wake hapa hata kama mpira una matokeo yake utagundua kwamba Namungo hawezi kutoboa hapa hata kama akijitunisha msuli vipi alihitaji kushushiwa mzigo huu wa lawama.

Namungo wamemaliza mwendo wao kinachoendelea sasa katika hatua waliyopo ni kuchukua uzoefu wa jinsi gani wanatakiwa kujipanga kiushindani wa Afrika zaidi ya walichofanya sasa.

Viongozi wa Namungo kuanzia mlezi wao mpaka hatua ya uongozi wao mkuu wanatakiwa kupongezwa kwa jinsi walivyofanya makubwa ya kuonyesha ushindani ,mkubwa katika msimu wa pili tu wa ligi ambao hata Simba na Yanga hazikuweza kufanya haya kwa haraka kaisi hicho.

Zipo timu ambazo katika mashindano haya ziliwahi kupoteza vibaya na kufikia hatua hata ya kushindwa kusafiri kwenda katika mchezo wa marudiano lakini haya yote licha ya uchanga wake lakini Namungo walisimama imara.

Ukiacha hilo kuna safari ambayo walikutana na misukosuko mikubwa waliposafiri kwenda Angola katika mchezo wa ugenini lakini hawakutetereka.

Hii ni ishara njema kwao kwamba hawa kama wakiendelea kupata usimamazi mzuri wanaweza kufanya makubwa katika kuipa nchi heshima.

Huu ni wakati sasa uongozi wa Namungo na hata wachezai na makocha wao kujifunza kitu kwamba kila kitu kiinawezekana kama utakuwa na malengo na kisha kuweka juhudi za kuyafanyia kazi malengo yako ili uvune matunda mengi.

Wapo wachezaji ambao hata hapa ndani walionyesha ushindani bora kama washambuliaji Stephen Sey, Sixtus Sabilo,kiungo Lucas Kikoti na hata kipa Jonathan Nahimana ambao hata huko Caf wakafanya kazi bora ambayo iliipa heshima klabu yao na hata Taifa kwa ujumla.Endapo Namungo watajifunza kitu wanaweza kurudi tena baadaye wakiwa na nguvu kubwa kuliko hiki ambacho wamekifanya msimu huu wa kwanza kwao katika mashindano ya Caf kwa kuwa uthubutu wao utabaki kuwa alama muhimu kwao.