UCHAMBUZI: Azam inahitaji tathimini pana ya wachezaji ilionao

Kwenye maisha unaweza kupewa kila kitu muhimu uweze kupata mafanikio, lakini kama utakosa akili iliyotulia malengo hayo yanaweza kuyeyuka na kujikuta ukianguka badala ya kupiga hatua ambayo ulitarajia.

Wakati mwingine hatua kama hiyo ya anguko hali ya kuwa una kila kitu inaweza kusababishwa na mambo mengi, lakini moja kati ya hayo ni maisha ambayo umeamua kuishi na kuendesha mambo yako muhimu.

Unaweza pia ukagundua kipi kimekuangusha, lakini pia usisahau kutoka katika eneo la anguko unahitaji msukumo mzito wa maamuzi kwamba eneo husika au mambo husika yakakukwamisha lazima ufanye juhudi za kutoka eneo hilo.

Hapa Tanzania kuna klabu moja ambayo maisha yake na kila kitu walichonacho hakiendani na mafanikio ambayo wamekuwa wakiyatafuta na sasa wanajikuta hata klabu ndogo nazo zikifanikiwa wao wakiwa papohapo walipo.

Hebu iangalie Azam FC, klabu ambayo ina karibu kila kitu ambacho kocha au hata mchezaji wanahitaji kuwa nacho. Hakuna maisha ya kubahatisha katika klabu hii, ina viwanja vyake, hosteli zake na Azam ina karibu kila kitu cha mazoezi ambacho watakihitaji kulea mchezaji.

Usiishie hapo Azam ina pesa ambazo kama wataamua hakuna klabu ya Simba wala Yanga wanaweza kushindana nayo katika kumpata mchezaji au hata kocha. Ndio sababu ni moja tu fedha wakati mwingine humaanisha kikubwa katika ushawishi.

Hebu tuangalie sasa uwekezaji wao unaendana na mafanikio? Jibu litakuja hapana ingawa wako ambao wanadhani Azam inaangushwa na kukosa idadi kubwa ya mashabiki, lakini binafsi napingana na hilo kutokana na sasa imekuwa ikipigwa vikumbo na hata klabu ndogo na mpya ambazo zimekuwa zikizaliwa.

Miaka miwili mfululizo ukiacha kuchukua taji la Ligi Kuu Bara ambalo limetua kwa klabu kubwa na kongwe Simba. Azam imekuwa ikikosa hata Kombe la Shirikisho Afrika.

Anguko hili sasa limekuwa likitanuka taratibu na sasa hata kukosa kombe ambalo kwao limezowea makabati yao la Mapinduzi.

Hapa lazima tuijadili kansa ambayo inazidi kuitafuna Azam ambayo ni maisha ya urafiki kati ya baadhi ya viongozi na wachezaji ambao naona kuna wachezaji wakubwa kuliko klabu.

Hii ndio Azam ambayo mchezaji anaweza kumwambia kocha kwamba hapa hutakaa na hatua hii - akaifanya kwa vitendo kwa kuamua kucheza kawaida na kisha baadaye kweli hilo likatimia na utaona kocha anaondolewa kweli.

Maisha hapa ni rahisi kwamba kuna uswahiba mkubwa kati ya viongozi na wachezaji ambao hii ni kansa mbaya ambayo itazidi kuitafuna Azam na kuzidi kuporomoka kadri siku zinavyosogea.

Azam sasa wana kocha mzuri mwenye rekodi kubwa katika soka la Afrika, George Lwandamina, lakini hata kama yuko pale anaweza asipate mafanikio ambayo angetamani kuyapata ndani ya klabu hiyo tajiri na akajikuta anajishangaa