SIO ZENGWE: Ule mjadala wa ‘timu kubwa’ umeishia wapi?

Derby hii kaziipo

Wiki chache zilizopita kulikuwa na mjafdala mkubwa usio na maana wa kujadili ukubwa wa timu, hasa Simba na Yanga.

Ulikuwa mjadala wa kutoana macho kwa jinsi wapinzani katika hoja hiyo walivyokuwa wakitoa povu kutetea wanachoamikni.

Hii ilitokana na mwenendo wa Simba katika michuano ya Afrika baaada ya kukaribia kuvuka kile kikwazo kikubwa kwa timu za Tanzania hivi sasa cha robo fainali. Baada ya Simba kufika fainali ya michuano ya CAF mwaka 1993, robo fainali imekuwa ndio kilele cha klabu zetu.

Mwenendo huo ulisababisha mashabiki wa Simba wqakiongozwa na ofisa habari wao kjutamba kuwa Simba ni miongoni mwa klabu kubwa barani Afrika na hilo likachagizwa na orodha ya ubora ya CAF inayoonyesha kuwa Simba ni moja ya klabu 20 bora.

Hakukuwa na tatizo la hoja hiyo kwa kuwa ni Dhahiri timu inapofanya vizuri Afrika, ni lazima itakuwa juu kwenye orodha ya ubora, hata kama itakuwa ‘klabu ndogo’.

Lakini wapinzani walipinga hoja hiyo, wakiongozwa na msemaji wa Yanga kwamba ukubwa wa timu hautokani na kufika robo fainali, bali kutwaa mataji, wakitoa mifano ya Bayern Munich, Real Madrid, Liverpool, Juventius na Al Ahly.

Ni moja ya mijadala inayochangamsha maongezi ya mpira wa miguu, lakini haisaidii mchezo huo kukua bali kufurahisha na mwisho wake mmoja kuonekana ‘ana akili sana’.

Kwa kuangalia tu suala la Bernard Morrisson unaweza kuona ni kwa vipi klabu zetu bado ndogo. Baada ya kuhusishwa katika tuhuma za uhalifu nchini Afrika Kusini, Morrison aliachwa na klabu yake ya Orlando Pirates.

Achilia mbali kuachwa, bali mchezaji huyo ni ‘wanted’ nchini Afrika Kusini na ndio maana alishindwa kwenda na Simba mar azote mbili klabu hiyo ilipoenda kucheza mechi za Afrika.

Klabu kubwa ni ile iliyojigtengenezea sera zake zinazolinda mienendo ya wachezaji ndani na nje ya uwanja. Kwamba hata mchezaji awe mzuri vipi, kama akikiuka sera hizo atakuwa hana nafasi kwenye timu.

Hilo ni moja ya mambo ambayo yanaweza kuifanya klabu ionekane kuwa kubwa, hata kama haina mafanikio barani Afrika au ndani ya nchi yake “kwa jicho la maendeleo”.

Winga wa Manchester United, Masson Greenwood ameondolewa kwenye timu hiyo baada ya kukubwa na kashfa ya kubaka. Yupo nahodha wa zamani wa Chelsea, Dennis Wise aliyetimuliwa na Leicester baada ya kumshambulia mchezaji mwenzake kwa masumbwi na kumvunja mfupa wa pua.

Patrice Evra alitimuliwa na klabu yake ya Olympique Marseille baada ya kupigana na masahabiki mwishoni mwa mechi na Adrian Mutu wa Chelsea alioomndolewa baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya cocaine—kumbuka si za kusisimua misuli!

Mshambuliaji wa zamani wa Sheffield, Ched Evans alitimuliwa baada ya kupatikana na hatia ya kubaka msichana wa miaka 19. Na wa mwisho katima orodha yangu ni Benjamin Mendy, beki wa kushoto wa Manchester City, ambaye amesimamishwa hivi sasa akikabiliwa na mashtaka kadhaa ya ubakaji na shambulio.

Haya ndiyo mambo yanayotakiwa kuibua mjadala ambao unasaidia klabu zetu kujiangalia mara mbili na kujitengenezea kanuni ambazo zitasaidia wachezaji wetu wawe na nidhamu binafsi ambayo husaidia timu kwa kiasi kikubwa.

Sera nyingine ni kama vile kuwa na program za vijana. Katika mwaka wake wa mwisho Real Madrid, Zidane alihangaika sana na uchovu wa wachezaji wake wane; Luca Modric, Toni Kroos, Casemiro na Thibaut Courtois.

Wakati huo nyota wengine walikuwa na majeruhi. Lakini kwa sababu klabu hiyo ina sera nzuri ya vijana, Zidane alipata ahueni kwa kuwa katika timu ya vijana kulikuwa na wachezaji ambao waliweza kuingia kikosini kucheza kwa dakika kadhaa na hivyo nyota hao wane kupata muda wa kupumzika.

Huku kwetu tunaomba mechi zisogezwe mbele ili wachezaji wapone majeraha au wapumzike ili tuwatumie kikamilifu mechi zijazo. Ukubwa wetu uko wapi?