Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

HISIA ZANGU: Operesheni Luanda na Nouakchott zimefanikiwa, tukutane Kwa Mkapa

Hisia Pict

Muktasari:

  • Bila ya Leonel Ateba maisha yangekuwa magumu Simba katika mechi mbili zilizopita. Na ni Ateba ndiye ambaye alimfutia kosa Che Malone juzi kwa kufunga bao muhimu. Kabla ya hapo wiki iliyopita alimbetulia pasi nzuri Jean Charles Ahoua aliyefunga bao dhidi ya CS Sfaxien.

TUANZIE wapi? Tukianza na Luanda, Angola tunaanza kukutana na kosa la Che Malone Fondoh. Imekuwa kawaida kwa sasa Che Malone kufanya makosa anayofanya. Zamani wakati anafika nchini hakuwa na makosa hayo. Sasa hivi imeanza kuwa mazoea.

Bila ya Leonel Ateba maisha yangekuwa magumu Simba katika mechi mbili zilizopita. Na ni Ateba ndiye ambaye alimfutia kosa Che Malone juzi kwa kufunga bao muhimu. Kabla ya hapo wiki iliyopita alimbetulia pasi nzuri Jean Charles Ahoua aliyefunga bao dhidi ya CS Sfaxien.

Che Malone asizoee tena makosa hasa katika mechi kubwa kama hizi. Katika Ligi Kuu Bara wanaweza wasitumie vyema makosa yako, lakini katika mechi kubwa hizi unakutana na wachezaji ambao wanaweza kutumia vyema makosa yako.


HIS 01

Na sasa Mnyama amepita kiulaini katika kundi lake la Shirikisho. Ingekuwa aibu kama asingepita. Mechi yake ya mwisho dhidi ya CS Constantine ambayo binafsi nilikuwa naihofia huenda ikawa ya kirafiki.

Hata kama Simba akifungwa halafu Bravos akamfunga CS Sfaxien, basi watafikisha pointi sawa na Simba, lakini Simba ana wastani mzuri katika mechi ambayo wamekutana wenyewe kwa wenyewe. Alishinda pale Temeke na ametoka sare Luanda.

Narudia kwamba ingekuwa aibu kwa timu kama Simba kutolewa katika michuano kama hii. Baada ya kubabaishana na wakubwa kina Al Ahly, Waydad Casablanca, AS Vita na wengineo katika miaka ya karibuni ingekuwa aibu kama wangetolewa katika pambano la awali na Al Ahly Tripoli ya Libya.

HIS 02

Ingekuwa aibu zaidi kama wangetolewa katika kundi lenye timu za Bravos, Constantine na Sfaxien ya Tunisia.

Sawa wanatoka katika mataifa makubwa ya Angola, Algeria na Tunisia, lakini Simba na watani zao Yanga walishapita katika hofu ya kucheza na timu za mataifa  makubwa. Na kwa Simba walishapita katika hofu ya kucheza na timu za nchi hizo ambazo zinashiriki Shirikisho.

Twende wapi? Nouakchott. Mji mkuu wa Mauritania, nchi ambayo ipo pembe fulani ya Afrika. Al Hilal ya Sudan wamehamishia mechi zao huko na kulikuwa na mtihani mkubwa kwa Yanga kwenda kusomba pointi tatu muhimu za kutanguliza mguu mmoja kwenda robo fainali za Ligi ya Mabingwa.

HIS 03

Yanga walijitakia wenyewe kuwa katika mazingira haya. Miezi michache iliyopita walikuwa Pretoria Kusini wakikaribia kabisa kuitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na kukaribia kutinga hatua ya nusu fainali. Kwanini miezi michache baadaye wajikute na pointi moja baada ya mechi tatu katika kundi lenye timu za TP Mazembe, MC Alger na Al Hilal ya Sudan?

Wakati Yanga wakionekana kuwa tayari kuiteka Afrika ghafla walianza kurudi nyuma miezi mitatu iliyopita huku wakifungwa hadi na Tabora United mabao 3-0 pale Mbagala. Wakayumba wakaachana na kocha wao, Miguel Gamondi kwa madai kwamba pamoja na wachezaji wake mastaa starehe zilikuwa zimewalevya.

Bahati mbaya kulevya kwao kwa starehe kuliingiliana na ratiba ya michuano hii mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu.

HIS 04

Wakachapwa Dar es salaam na Al Hilal. Wakachapwa ugenini na MC Alger. Prince Dube akaipatia Yanga pointi ya kwanza pale Lubumbashi katika dakika za jioni.

Na sasa Yanga ikawa na ulazima wa kushinda mechi zake tatu zilizobaki. Mbili Dar es salaam na moja kule Mauritania. Ilishinda moja ya Dar es salaam dhidi ya TP Mazembe halafu ikawa na mechi hii hapa mkononi  dhidi ya Al Hilal pale Nouakchott. Haikuwa mechi rahisi.

Bahati nzuri Yanga wamerudi kuwa walewale waliokuwa moto kabla ya kundi hili kuanza. Fomu yao katika kundi ilipotea katika wakati mbaya na imerudi katika wakati mzuri.

HIS 05

Kama Yanga wangekuwa katika fomu hii  katika mechi za awali kusingekuwa na timu ya kuwahangaisha.

Aziz Ki alimaliza pambano la juzi mapema tu kwa kupiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja katika nyavu za Al Hilal. Hii ndio silaha yake kubwa uwanjani. Anaweza asiwe fomu, lakini akaleta vipindi vyake vya maajabu. Sio mara ya kwanza. Amefanya hivyo mara nyingi na hata ugenini aliwahi kufanya hivyo dhidi ya Club Africain ya Tunisia.

Yanga walikuwa vizuri katika kila idara juzi. Wangeweza kufunga mabao mengi, lakini hawakuweza. Hata hivyo hilo halikuwa jambo muhimu zaidi ya kulilinda bao la Aziz. Na walilinda vyema.

Kocha, Saed Ramovic anaonekana kuanza kuijua timu yake. Hata ‘sub’ yake ya kwanza alikuja kuifanya dakika ya 87 wakati Aziz Ki alipompisha Kennedy Musonda. Inaonekana pia anajua namna gani ya kuwatumia washambuliaji wawili, Clement Mzize na Prince Dube kwa wakati mmoja.

HIS 06

Hatujui timu yake itaendelea kuwa hivi kwa muda gani wakati huu Clatous Chama akiwa amerudi na Maxi Nzengeli akiwa anakaribia kurudi. Tunachojua ni kwamba Yao Kouassi atarudi katika nafasi yake pindi akipona na Yanga itaendelea kukamilika.

Lakini sasa wana mechi ya machozi, jasho na damu dhidi ya MC Alger katika Uwanja wa Mkapa pale Temeke. Waliwahi kucheza mechi ya namna hii wakati walipotakiwa kuichapa CR Belouzidad mabao manne na kwenda hatua ya robo fainali na kweli walifanya hivyo. Joseph Guede aliziona nyavu za Belouzidad katika dakika za jioni.

Na sasa ni zamu ya kina Dube kufanya hivyo katika pambano hili la machozi, jasho na damu dhidi ya MC Alger ambao wanafahamu kuwa wanakuja vitani.

Wakati mwingine Yanga na Simba zimezoea kujiweka katika mazingira magumu kisha zinajinasua. Yanga wana kazi chafu mkononi mwao Jumamosi ijayo.

Kwanza wanatakiwa wajae uwanjani kuipa mazingira magumu MC Alger. Pili wanatakiwa wapambane hasa kujaribu kupata bao au mabao ya mapema. Waarabu watajaribu kucheza kwa akili kubwa ya kujihami mpaka pale watakapotangulia ndipo watagundua kwamba matokeo ya kufungwa hayasaidii. Wataondoka langoni mwao.

Vinginevyo watapoteza muda kadri watakavyoweza. Watajaribu kujihami kwa usahihi kadri watakavyoweza. Kisoka, narudia kwamba katika kundi hili hakukuwa na timu ya kupambana na Yanga kabla ya Yanga kupoteza fomu yake chini ya Gamondi. Ni Yanga wenyewe wamejitakia kuwa katika mazingira haya. Tukutane Lupaso Jumamosi.