DATA ZAKE: OZIL: Pesa inamwondoa Arsenal

Tuesday December 05 2017
ozil

KITENDO cha Mesut Ozil kwenda kuwakumbatia makocha wa Manchester United baada ya mechi ya Jumamosi iliyopita huko Emirates imezua utata huko Ulaya. Si unajua, mchezaji huyo yupo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Arsenal na bado hajasaini dili jipya na wala haonekani kufanya hivyo, hivyo kitendo hicho kimepata tafsiri ya moja kwa moja kwamba anajiandaa mapema kabla ya kwenda kuungana nao huko Old Trafford mwishoni mwa msimu.

Kuna taarifa zinazodai Ozil anawindwa na Man United na Kocha Jose Mourinho hakukataa kama kweli hana mpango wa kuipata saini ya Mjerumani huyo, ambaye kimsingi anamtaka kwa sababu kikosi chake kwa sasa hakina Namba 10 wa maana mwenye uwezo wa kuichezesha timu kwa ubunifu inapohitajika kufanya hivyo.

Kama kwenda au kutokwenda, basi Ozil hawezi kukubali tu kizembe. Mpango wowote ambao utamwondoa Arsenal kwenda kwenye timu nyingine kwanza utazingatia pesa.

Ozil anatafuta pesa, ndiyo maana hata kwenye mpango wa kuzungumzia dili jipya amekuwa akimlazimisha Kocha Arsenal Wenger amlipe mshahara unaoanzia Pauni 250,000 kama si Pauni 300,000 kwa wiki.

Mourinho anaweza kulipa mshahara huo kama anavyofanya hivyo kwa mastaa wengi pale Man United, akiwamo Romelu Lukaku akipokea pesa ndefu kabisa.

Rio Ferdinand, beki wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England amemwambia Mourinho aende kumchukua Ozil bila ya kusita.

Advertisement

Ozil ni mtu wa familia. Baba yake anaitwa Mustafa na mama yake ni Gulizar. Dada yake anaitwa Dugyu na mwingine ni Nese, wakati mdogo wake anaitwa Mutlu Ozil. Ozil rafiki yake mkubwa ni Lukas Podolski.

UDHAMINI: Dola 6.5 mil Anazovuna kwa mwaka kwa dili za kibiashara Dola 35 milioni udhamini wake kutoka Kampuni ya Adidas.

MCHUMBA WAKE: SIKU za karibuni, Ozil ameripotiwa kunasa kwenye penzi la Miss Uturuki 2014, Amine Gulse. Kabla ya hapo, Ozil alikuwa kwenye penzi la mrembo Mandy Capristo, mwanamuziki huyu wa huko Ujerumani.

MAKAZI YAKE: Jumba la Dola 4 milioni huko London, England. Lina kila kitu ndani ikiwamo bwawa la kuogelea. Ozil aliripotiwa kutaka kununua jumba la Pauni 5 milioni huko Istanbul, Uturuki. Ozil amenunua pia jumba la Pauni 10 milioni jirani tu na nyumba aliyokuwa amepanga.

USAFIRI WAKE: Ozil ni mpenzi wa magari ya kifahari.Baadhi ya magari yake ni Mercedes Benz SLS AMG yenye thamani ya Dola 221,580. Anamilini Ferrari kibao pia.

Ozil anaripotiwa kuwa na kipato cha Dola 50 mil ndiyo utajiri wake

THAMANI YAKE: Dola 63 milThamani ya miaka yake mitano akiwa na Arsenal.

Mwaka 2013, Arsenal ililipa Dola 65 milioni kupata saini yake.

Advertisement