Zuchu amzawadia gari mama yake

Hatimaye nimemnunulia mama yangu gari lake pendwa.Hayo ndio maneno ya msanii, Zuhura Othuman, maarufu Zuchu baada ya kutimiza ndoto za kumnunulia mama yake gari.
Zuchu ni mtoto wa mwimbaji taarabu wa siku nyingi Hadija Kopa.
Zuchu ameonyesha jana Jumatano Juni 16, 2021 tukio hilo la kumkabidhi gari mama yake huyokupitia  ukurasa wake katika  mtandao wa  Instagram tukio hilo la kumkabidhi mama yake huyo.
Gari hiyo aina ya Alphard, Zuchu anasema ilikuwa ni gari yake pendwa  ambapo alionyesh pia video alivyokuwa akimuuliza kwa  nini anapenda gari hiyo, aliyomrekodi mwezi mmoja uliopita.
“Nina furaha mno miezi 12 iliopita sikua na uwezo hata wa kumlipia nauli mama yangu. Allah akuweke uzidi kula matunda yako mama unastahili zaidi ya hili mama yangu .
Mwenyezi mungu atujaalie sote uwezo wa kuwatunza wazazi wetu amen. Nakupenda mama.
Kwa upande wake Hadija Kopa alimuombea Zuchu Mungu amjalie na kumuongezea pale alipopungukiwa.