Zuchu aja na singeli

Msanii kutoka lebo ya wasafi, Zuhura Omar maarufu kwa jina la Zuchu ameachia wimbo wake mpya ukiwa katika mahadhi ya singeli.
Wimbo huo ameuachia leo Jumanne Juni 15, 2021, ambao kaupa jina la ‘Nyumba Ndogo’.
Ujio wa wimbo huo alianza kuutangaza tangu jana na baadhi ya maneno aliyokuwa akiwauliza mashabiki wake kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ni pamoja na kuwataka waseme ‘SU’ ilii auchie.
Ndani ya wimbo huo Zuchu anaeleza kuwa yeye ni mke mweza asiye na ubaya.
Zuchu kutoa wimbo wa singeli atakuwa msanii wa tatu ndani ya lebo ya WCB kufanya hivyo, akitanguliwa na Lavalava aliyeimba wimbo wa Wanga kwa kushirikishwa na msanii wa singeli Meja Kunta uliotoka februari mwaka 2020.
Wimbo huo ukiwa haujapoa Machi mwaka huohuo msanii Rayvanny naye akaachia Miss Buza ukiwa katika mahadhi hayo ya singeli ambao mpaka sasa umeshatazamwa zaidi ya mara milioni 8.