YouTube yafunga akaunti ya Diamond Platnumz, Wasafi waeleza sababu

YouTube yafunga akaunti ya Diamond Platnumz, Wasafi waeleza sababu

Mtandao wa YouTube wa msanii, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' ulikuwa haupatika toka jana April 24 na uongozi wa Wasafi umeeleza sababu za kutopatikana.

Akizungumza na Mwanaspoti leo Jumatatu Aprili 25, 2022 Mkuu wa masuala ya kidijitali wa kampuni hiyo, Ackim Ndolo amesema kilichotokea ni watu kudukua mtandao huo toka jana.

Ndolo amesema baada ya kuudukua, watu hao walitumia mtandao huo kurusha maudhui ambayo yapo kinyume na mwongozo wa YouTube.

"Walipodukua walirusha live masuala ya sarafu za kidigital maudhui ambayo ni kinyume na miongozo ya mtandao huo wa YouTube," amesema Ndolo.

Hata hivyo ameeleza kuwa kutokana na hilo, uongozi walitoa taarifa youtube ambayo nayo iliifunga mara moja.

Ametumia fursa hii kuwaomba mashabiki wa Diamond kuwa watulivu wakati suala hilo linafanyiwa kazi na kuahidi itarejeshwa muda sio mrefu.

YouTube ya Diamond ilianzishwa mwaka 2012 na mpaka sasa ina zaidi ya wafuasi 'subscribers' milioni sita.