Vanessa aibukia kwenye wimbo wa Rotimi

Vanessa aibukia kwenye wimbo wa Rotimi

Muktasari:

IKIWA imepita miezi mitatu tangu mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee atangaze kuachana na ishu za muziki, staa huyo ameibukia kwenye wimbo mpya wa mpenzi wake, Rotimi ulioachiwa leo Jumanne Disemba 1, 2020.

IKIWA imepita miezi mitatu tangu mwanamuziki wa Tanzania, Vanessa Mdee atangaze kuachana na ishu za muziki, staa huyo ameibukia kwenye wimbo mpya wa mpenzi wake, Rotimi ulioachiwa leo Jumanne Disemba 1, 2020.

Katika video ya wimbo huo wa mapenzi uliopachikwa jina la Love Someday, Vanessa Mdee ameigiza kama mpenzi wa Rotimi ambaye pia ni mwanamuziki.

Wimbo huo umetoka kwenye kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rotimi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo mwenye makazi yake Marekani, amesisitiza kwamba ngoma hiyo ni namna ya kusherehekea siku yake na mpenzi wake, akimaanisha Vanessa.

“Hakuna namna nzuri ya kusherehekea siku yangu zaidi ya kusambaza upendo kwa wimbo mzuri pamoja na kuwa na mwanamke wangu mzuri,” ameeandika Rotimi kwa lugha ya Kiingereza

Kwa upande wa Vanessa, ameandika mkeka mrefu wa kumtakia kheri ya kuzaliwa mpenzi wake ikiwa ni pamoja na kuelezea ni jinsi gani mapenzi ya mwanaume huyo yalivyoboresha maisha yake.

Hii si mara ya kwanza kwa Vanessa kuigiza kwenye video ya wimbo wa mpenzi wake, kwani mwaka 2017 aliigiza kwenye wimbo wa aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Juma Jux, wimbo unaoitwa Sisikii.

Na KELVIN KAGAMBO