Tanasha Donna atarajia kupata Sh2.3 bilioni

Tuesday August 02 2022
tanasha pic
By Rukia Kiswamba (SJMC)

STAA wa muziki na mwanamitindo kutoka Kenya, Tanasha Donna ameweka wazi kwamba mpaka atakapofikisha miaka 30 atakuwa amepata sh2.3 bilioni kutokana na shughuli anazozifanya mbali na muziki.

Mwanamitindo huyo amesema hayo wakati akifanya mahojiano na moja ya kituo cha radio cha nchini kenya.

Amesema mbali na muziki zipo shughuli zingine anazowekeza ambazo zinaweza kumuingizia Dola 1milioni kabla ya kufikisha umri huo.

Tanasha amesema licha ya kuwa mwanamuziki ila amewekeza kwenye biashara japo hataki kuonyesha vitu anavyovifanya kwa umma.

Msanii huyo amesema; "Kabla ya kufikisha miaka 30 kwa mipango na neema ya Mungu Inshaalah nitatengeneza mamilioni ya fedha japokuwa napenda sana muziki lakini nitajiingiza kwenye biashara,"

Tanasha (27) anatamba na nyimbo kadhaa zikiwemo Mood, La Vie aliyomshirikisha Mbosso na Ride aliyoimba na rapa wa Hip Hop Khaligraph Jones.

Advertisement
Advertisement