Switzerland, Norway zamwaga mabilioni kusapoti wasanii Tanzania

Switzerland, Norway zamwaga mabilioni kusapoti wasanii Tanzania

Muktasari:

  • Zaidi ya sh3 bilioni zimetolewa na nchi ya Switzerland na Norway kwa ajili ya kusaidia kuendeleza  wasanii Tanzania.

Dar es Salaam. Zaidi ya Sh3 bilioni zimetolewa na nchi ya Switzerland na Norway kwa ajili ya kusaidia kuendeleza na kukuza vipaji vya wasanii Tanzania, Katika fedha hizo Switzerland imetoa Sh2.1 bilioni huku Norway wakitoa Sh1 bilioni.
Akizungumza katika hafla ya kutuliana saini ya kupokea fedha hizo,Mkurugenzi wa Nafasi Arts Space,Rebecca Corey,amesema fedha hizo zitatumika katika mfuko wao  unaojulikana kwa jina la Sanaa Huru'Sanaa Feel Free' ambao huwapatia fedha wasanii mbalimbali wanakuja na maandiko mazuri ya kiununifu ya kuyafanyia kazi.
"Fedha hizo tumekuwa tukizitoa kwa makundi au msanii mmojammoja atakayeandika andiko zuri la kufanya katika sanaa yake lengo likiwa kuieleimisha jamii kupitia vipajo vyao.
"Hii inahusisha wasanii wote kutoka Tanzania na wanaofanya aina yoyote ya sanaa,"amesema Mkurugenzi huyo.
Katika andiko hilo,Rebecca amefafanua kuwa  watakaofanikiwa kushinda  watapatiwa fedha  kati ya Sh10 milioni hadi Sh50 milioni kutegemea na ukubwa wa mradi husika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa Nafasi Paul Nduguru, amesema tofauti na maombi kwa fedha nyingine hizi msanii anaachwa kuwa huru kuchagua wazo lake lolote analolipenda kulifanyia kazi na hivyo kusaidia kutimiza ndoto za wasanii wengi.
Mwakilishi kutoka  ubalozi wa Switzerland,Leo Nascher, amesema ni miaka miaka 17 sasa nchi hiyo imekuwa ikisaidia Tanzania katika masuala ya sanaa na wana uhakika mradi wa 'feel free' utasaidia wasanii kuendeleza vipaji vyao.
Naye mwakilishi kutoka ubalozi wa Norway,Kjetil Schie  amesisitiza uwepo wa uhuru kwa msanii kueleza kile kilicho na kutaka kuheshimiwa kwa  masuala ya haki za binadamu.