Rose Manfere kutoshiriki Miss World, sababu yatajwa

Rose Manfere

Muktasari:

  • Kamati ya Miss Tanzania imevunja mkataba na mlimbwende wa Tanzania  mwaka 2020,  Rose Manfere baada ya kukiuka baadhi ya masharti ya  mkataba.

Dar es Salaam. Kamati ya Miss Tanzania imevunja mkataba na mlimbwende wa Tanzania  mwaka 2020,  Rose Manfere baada ya kukiuka baadhi ya masharti ya  mkataba.

Manfere hataweza kushiriki mashindano ya urembo wa dunia yanayotarajiwa kufanyika Desemba 2021  nchini Puerto Rico na badala yake aliyekuwa mshindi namba mbili, Juliana Rugimisa ataliwakilisha Taifa.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Julai 14, 2021 na mwakilishi wa kamati ya mandaalizi ya mashindano hayo, Azama Mashango alipozungumza na Mwananchi Digital amesema Manfere amefanya makosa yaliyopelekea kuvunja mkataba wake.

“Manfere bado ni miss Tanzania hajavuliwa taji, kuna makosa yalitokea amevunja mkataba lakini maamuzi ya kamati yameona kwamba asivuliwe taji lakini asiwe mwakilishi wa Tanzania kwenye Miss World kwa mwaka huu, Juliana ataenda kama mwakilishi wa Miss World Tanzania kwani mkataba unasema mshindi wa kwanza akishindwa kutekeleza majukumu yake kama mkataba unavyomwambia mshindi wa pili ndio atakuwa mwakilishi wa Miss World Tanzania, lakini Manfere bado ni Miss Tanzania, " amesema.

Rose Manfere kutoshiriki Miss World, sababu yatajwa

Ufafanuzi huo umekuja baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Rose amevuliwa taji.