Rich Rich: Basata ichukuwe kodi michoro ya SGR

Muktasari:

Michoro yote ni Sanaa,nadhani ifike mahali kodi yake ielekezwa Basata,fedha ambazo zitasaidia kuwafanyia mambo mbalimbali wasanii.

MSANII wa filamu nchini Tanzania, Single Mtambalike maarufu Rich Rich amependekeza michoro yoyote kodi yake ipelekwe Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Rich ambaye kwa sasa ni diwani wa Kawe, ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 2, 2020 katika kikao kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo na  wasanii wa filamu na sanaa za maonyesho, kilicholenga kupokea maoni ya namna ya kuendeleza sekta ya filamu nchini.

Akitoa maoni yake, Rich amesema amefanya kazi na taasisi zinazosimamia sanaa ikiwemo Basata ambapo yeye ni mmoja wa wajumbe wa bodi yake na kubaini kuwa kinachowafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao ni ukosefu wa fedha licha ya kuwa wana vyanzo vingi vya ukusanyaji mapato.

Akitolea mfano Rich amesema katika kila mchoro unaoonekana kwenye majengo yakiwemo mabango ya matangazo, maghorofa, miradi mikubwa ya serikali kama Reli ya Ummeme (SGR), mradi wa kufua umeme Rufiki, vyote hivyo  ni sanaa.

"Michoro yote ni sanaa, nadhani ifike mahali kodi yake ielekezwa Basata, fedha ambazo zitasaidia kuwafanyia mambo mbalimbali wasanii badala ya kulaumu kwamba hawana msaada na wasanii zaidi ya kuwafungia kazi zao wakati bajeti hiyo hawana," amesema.

Amesema eneo lingine ambalo Basata wanaweza kukusanya pesa ni katika kumbi za starehe ambapo pesa hiyo yote kwa sasa inaenda Halmashauri na Manispaa.

"Hawa ni kiasi cha kuwezeshwa namna ya kufika katika kumbi hizo na kukusanya fedha kwani ni eneo linalowahusu kwa kuwa kule ni burudani zinatolewa na wasanii sasa kwa nini pesa wachukue Manispaa,?" alihoji Rich.

"Ukiachilia baa, pia vigodoro na sherehe mbalimbali za mtaani ni mahali  ambapo Basata inaweza kupiga pesa, nilienda Zanzibar kujifunza na kukutana na jambo hili.

" Kwa nini tusifanye hivyo, kwani kwa siku hapa Dar vinaweza kupigwa vigodoro hata 600, ukikusanya kila kimoja 50,000 ni pesa nyingi za kuendesha Basata na kuacha kutegemea kila kitu kutoka serikalini," amesema.

Akijibia hilo, Dk Hassan Abbas ameagiza Bodi kwenda kuweka masuala hayo kwenye kanuni zao na kuona namna gani litafikishwa ngazi za juu kwa ajili ya utekelezaj