Pozi picha la Diamond na Zari laibua gumzo

Monday May 03 2021
pichaaa pic
By Nasra Abdallah

Saa chache baada ya meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam kutupia picha ikimuonyesha msanii huyo akiwa katika pozi kali la kimahaba na Zari, picha hiyo yaibua gumzo.

Sallam alitupia picha hiyo jana Jumapili Mei 3, 2021 katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ambapo Diamond aliyekuwa amevalia nguo nyeupe akionekana kumuwekea mkono begani Zari aliyekuwa amevalia nyekundu na kumuegemea msanii huyo, maeneo ambayo yanaonekana wapo jiokoni.

Pembeni yao alikuwepo Sallam akiwa ameshikilia glass ya juisi,ambapo wote walionekana katika mkao wa pozi la kupiga picha.

Aidha Sallam katika picha hiyo, Sallam alimtag mpigapicha wa Diamond anayejulikana kwa jina la Lukamba hii ikiwa imepita siku chache tangu mpigapicha huyo  kuhoji kutoonekana kwa Sallam huko Afrika Kusini ambapo Diamond yupo kwa ajili ya shughuli za kuandaa albamu yake ya tatu, ambapo pia amefika nyumbani kwa Zari kusalimia watoto.

Hata hivyo gumzo la picha hizo linakuja ikiwa wawili hao kila mmoja kwa wakati wake alisema wameamua kubaki kama wazazi kulea watoto.

Kama haitoshi ni hivi karibuni Zari alimuonyesha mpenzi wake mpya anayejulikana kwa jina la Blackkstallio, ambaye alikuwa akiweka picha wakiwa wanakula naye bata maeneo mbalimbali.

Advertisement

Baadhi ya watu walioona picha hiyo akiwemo Hajzo_Dripboi ameandika”Kwani jamani simwezi wa ramadhan huu .

Wakati Tijara Mwihaki ameandika”Warudiane aki”.

Mtheice yeye ameandika”Jamani ili penzi mbona lina baraka nyingi shida nini,Diamond Platnumz unafeli wapi?,”.

Chomoani Jambe4530 ameandika”Si mke wa mtu huyu,”.

Advertisement