Nandy aingia kama zawadi Uwanjani

Sunday August 29 2021
nandy pic 1
By Ramadhan Elias

MSANII wa kizazi kipya Nandy ameingia kama zawadi  kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuanza kuimba huku mashabiki wakishusha shangwe la kutosha.

Nandy aliingia akiwa amebebwa kwenye kibanda kilichotengenezwa kwa kiboksi cha zawadi ‘GiftBox’ huku akitanguliwa na madansa wake wa kiume na wakike waliokuwa zaidi ya 10.

Baada ya kufika eneo la kukimbilia la uwanja  ambapo ni karibu na jukwaa, walimshusha chini taratibu na kulifungua boksi lile lililokuwa limefungwa kwa utepe wa kijani na njano kisha Nandy kuonekana na kuanza kuimba.

Staili hiyo ya kuingilia iliwainua vitini mashabiki wa Yanga waliojaa uwanjani hapa na kuanza kumshangilia huku akiimba nyimbo ya Yanga na waksti huo madansa wake walikua wakikiwasha jukwaani huku yeye akizunguka uwanja mzima.

Baada ta hapo alipiga nyimbo zake nyingine mbili kisha kushukuru na kuondoka.

Advertisement