Kwani Zuchu anasemaje na Olakira

Monday May 03 2021
zuchuu pic
By Nasra Abdallah

NI siku saba zimepita tangu nyimbo mbili za lebo tofauti zilizo na ushindani zitoke ndani ya siku moja.

Nyimbo hizo ni ile ya Attitude ya msanii Harmonize kutoka lebo ya Konde Gang na Olakira ya Zuchu kutoka lebo ya WCB.

Wakati Harmonize katika wimbo wake huo amemshirikisha mwanamuziki wa DR Congo, Awilo Longomba na yule wa Bongo Fleva H.Bab, Zuchu amekimbilia, Nigeria na kuimba na msanii Sere.

Hata hivyo, ukija upande wa viewers watu ambao wasanii sasa hivi ndio wanashindana kuwa nao kwenye mitandao ya kuuzia muziki, wimbo wa Attitude ndio unaonekana kutazamwa zaidi kwani mpaka juzi ulikuwa umetazamwa mara 6 milioni.

Upande wa Olakira kwa siku hiyo, ulikuwa haijafikisha watazamaji hata milioni moja kwani ulikuwa na takribani viewers 864,000.

Jambo hili linazua maswali kwa nini imekuwa hivyo, ukizingatia Zuchu licha ya uchanga wake amekuwa mmoja wa wasanii ambao nyimbo zao zinapendwa na zinapata sapoti ya kutazamwa.

Advertisement

Msanii huyo ambaye ni mtoto wa mwimbaji taarabu, Hadija Kopa, akiwa na mwaka mmoja tu kwenye sanaa hiyo nyimbo zake zisizopungua 10 hadi sasa alizozitoa, hakuna hata moja iliyokuwa na viewers chini ya milioni tano.

Je nini kimemtokea safari hii, tunaweza pia kumuuliza kwani yeye mwenyewe anasemaje?

Advertisement