Kwa Mpalange yamponza Muumini Mwinjuma

Mwanamuziki wa dansi, Muumini Mwinjuma, naye amejikuta mikononi mwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kutokana na wimbo wake wa Kwa Mpalange aliouchia hivi karibuni.
Muumini aliitwa katika baraza hilo Aprili 15, 2021 siku ambayo pia ndiyo aliyoitwa msanii Baba Levo na kuitikia wito kwa kufika katika ofisi zao zilizopo maeneo ya Ilala Sharif Shamba.
Akizungumza na Mwanaspoti, Muumini amesema alipigiwa simu na kulezwa kuwa wimbo wake wa Kwa Mpalange na shida.
“Nilipigiwa simu jana (Jumatano), na kuelezwa kutakiwa kufika Basata na nimeitikia wito lakini kubwa ni wimbo wangu wa Kwa Mpalange, hivyo nitawasikiliza maelekezo watakayonipa maana si unajua Basata ndio mlezi wetu,” amesema Muumini.
Amesema ameutoa katika kuwapa burudani mashabiki zake ukiwa katika mahadhi ya singeli.
Kwa sasa Muumini ambaye aliwahi kutesa na nyimbo mbalimbalii kiwemo Kilio cha Yatima, Mgumba amezaa na Tunda, ameirudisha tena bendi yake ya Tamtam.