Kofii atua kwenye mgawahawa wa Shilole Dar

Wednesday November 25 2020
kofiolomide pic

Unaweza usiamini lakini ndio hivyo, msanii mkubwa barani Afrika, Koffi Olomide ametinga katika mgawa wa  Shilole na kumuacha na mshangao msanii huyo wa nyimbo na maigizo nchini

Koffi  alifika katika mgahawa huo uliopo maeneo ya Kinondoni jana Jumanne Novemba 24 na kupokelewa na mwenyeji wake Shilole, ambaye alionekana kutoamini anachokiona machoni mwake.

Msanii huyo kutoka nchini DRC Kongo,  yupo nchini kwa mualiko wa msanii wa Bongo Fleva,Diamond Platnumz kwa ajili   ya shughuli zao kimuziki, na tayari wameshaingia studio kutengeneza nyimbo.

Katika ukaribisho huo, Shilole kama kawaida yake hakuona aibu kuongea kingereza chake cha kuunga unga kwa Koffi ambaye anazungumza zaidi kilingala, kifaransa na kingereza,.

Akizungumzia tukio hilo  kupitia ukurasa wake  wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Shilole ameandika “Kwanza nakushukuru Diamond kwa kunitangazia Shishi food yangu, kwani wasanii wakubwa ukiwaleta lazima uwaambie kuwa nina dada yangu muimbaji na mjasiriamali mwenye mgahawa wenye chakula kitamu chenye asili ya Afrika.

“Asante sana karibu sana Koffi Olomide_ msinicheke na ngeli yangu mwenyewe nimepambana balaa,”ameandika Shilole.

Advertisement

___________________________________________________

By NASRA ABDALLAHAdvertisement