Kajala, Harmonize wachorana tattoo

Friday February 19 2021
kajala pic
By Nasra Abdallah

PENZI la msanii wa filamu, Kajala Masanja na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize linazidi kupamba moto na sasa wamefikia hatua ya kuchorana tattoo.

Wawili hao walianika pezi lao kwa mara kwanza siku ya wapendao Februari 14,2021 wakiwa visiwani Zanzibar wakiponda raha maeneo mbalimbali.

Pia katika sakata la kuvuja kwa picha za mtoto wa Kajala, Paula hivi karibuni  na msanii Rayvanny, Harmonize ameonekana akiwa mstari wa mbele na kuonekana naye mara kwa mara vituo tofauti vya Polisi Kawe ambapo  Kajala alipopeleka malalamiko yake na kuhojiwa.

Hata hivyo wawili hao wameachia video na picha ikiwaonyesha wamechorana tattoo shingoni.

Wakati tattoo ya Kajala ikiwa na kofia ya kifalme katikati kukiandikwa herufi H, na chini alama ya karata ya jembe, Harmonize yake ina kofia ya malkia katikati ikiwa na herufi K na chini alama ya karata ya kopa.

Advertisement