Dogo Janja agoma kupimwa corona akitokea Afrika Kusini

Muktasari:

Wakati msanii huyu akigoma kupima Corona, mwongozo wa Wizara wa afya unamtaka kila mtu aliyetoka nje ya nchi kupima hata kama kapima nchi aliyotoka huku wale wanaotoka nchi ya India watalazimika kuwekwa karantini kwa siku 14.

Msanii wa muziki wa Bongo Fela, Dogo Janja amegoma kupimwa ugonjwa wa corona mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Dogo Janja ambaye jina lake halisi ni Abdulaziz Abubakar’, alikuwa ametokea nchini Afrika Kusini, ameliweka wazi hilo jana Alhmisi Mei 7, 2021 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter.

Amendika”Hii nchi Tanzania bado ina uonevu wa kishamba sana, sidhani kama mama yetu Rais Samia Suluhu anafahamu.. muda huu nafika uwanja wa ndege wa kimataifa nikitoea Afrika Kusini na Afrika Kusini huko  nimepima na nina majibu ya  Corona. Lakini hawayataki wanataka hela kutupima upya.

“Sasa ndugu zangu wa Tanzania mimi nina hela lakini sitoi hata kumi.. mniletee uji kituo nitachokuwepo nikikosekana hewani shughulikeni na Polisi w uwanja wa ndege,”ameandika Dogo Janja.

Hata hivyo wakati msanii huyu akigoma kupima corona, mwongozo wa Wizara wa afya unamtaka kila mtu aliyetoka nje ya nchi kupima hata kama kapima nchi aliyotoka huku wale wanaotoka nchi ya India watalazimika kuwekwa karantini kwa siku 14.

Kwa wale wanaosafiri kwenda nje gharama zake dola 100 sawa na Sh230, 000 wakati kwa wale wanaoingia ni dola 25 sawa na Sh57.9.