Diamond, Alikiba kesho hapatoshi

Wednesday July 28 2021
kiba pic
By Nasra Abdallah

Wasanii nyota wa Tanzania Diamond Platnumz na Alikiba kesho Julai 29 hapatoshi YouTube.
Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mastaa hawa wawili wa muziki wa Bongofleva, nchini kutangaza kuachia video za nyimbo zao mpya.
Hilo wamelieleza leo Jumatano Julai 28, 2021 kwa nyakati tofauti kupitia kurasa zao kwenye mtandao wa Instagram kutangaza jambo hilo.
Wakati Alikiba akiachia video ya wimbo wa ‘Jealous’, Diamond yeye ataachia ile ya wimbo IYO.
Kwa upande wa Diamond ameandika” Video kesho saa nne asubuhi, Alikiba yeye ameandika “JeAlous inatoka Alhamis hii".
IYO ya Diamond aliyoimba katika mtindo wa Amapiano, aliuachia Julai 15 kwa kuwashirikisaha wasanii wa nchini Afrika kusini Mapara A jazz na Ntosh Gazi.
Huku Alikiba wimbo wake wa Jealous ameimba kwa kumshirikisha Mayorkun msanii kutoka Nigeria na aliuachia Julai 22.
Nyimbo hizo mbili mpaka sasa zinafuatana kwa kutazamwa huko youtube ambapo Iyo inashika namba nane na Jealous ikishika namba tisa.

Advertisement