Barnaba anogesha tuzo za TFF

Thursday October 21 2021
barnaba pic
By Ramadhan Elias

MSANII wa muziki wa Bongofleva, Barnaba Classic amenogesha usiku wa Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa kutumbuiza mubashara nyimbo mbalimbali.

Barnaba ambaye anasifika kwa kutimbuiza mubashara amepanda stejini muda mchache baada ya mgeni rasmi wa hafla hiyo inayoendelea katika Ukumbi wa JNICC, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kumaliza kutoa tuzo kwa timu zilizobeba mataji ya msimu uliopita.

Barnaba ameimba nyimbo mbili ambazo ziliwaburudisha wadau waliopo ukumbini kisha kushuka akipigiwa makofi na ratiba nyingine kuendelea.

Advertisement