Aunt Ezekiel bila watoto watatu hamuachii Kusah

Muktasari:

Msanii wa Bongomovie, Aunt Ezekiel, amesema mzazi mwenzie Kusah hatakubali abanduke mikononi mwake bila watoto watatu.

Msanii wa Bongomovie, Aunt Ezekiel, amesema mzazi mwenzie Kusah hatakubali abanduke mikononi mwake bila watoto watatu.

Aunt ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 16, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari namna alivyopata tabu kupata watoto akiwemo huyu wa pili.

Aunt na Kusah ambaye ni msanii wa muziki wa Bongfleva,mwaka huu wamejaliwa kupata mtoto mmoja,mahusiano ambayo awali yalikuwa ya siri na kuna kujulikana mpaka pale alipotoka arobaini.

Hata hivyo msanii huyo amesema kutokana na namna alivyohangaika hadi kuanza kutumia dawa, amesema hatakubali kutoa nafasi ya muda mrefu,kubeba mimba mingine.

"Nimejipangia kuwa na watoto wanne na sasa itakuwa ni bandika bandua ambapo huyu mdogo akifikisha mwaka tu nabeba mimba ingine.

"Pia ni katika kutaka kuzaa na baba huyohuyo kwa kuwa nimegundua tunapowapa nafasi ndipo yanapoingia mambo mengine na kujikuta tunaanza kuchanganya wababa,"amesema Aunt.

Kwa mtoto wake wa kwanza anayejulikaana kwa jina la Cookie amesema alitamani ambebe mimba akiwa na miana mutatu lakini matokeo yake ilifika hadi sita ndio akafanikiwa kupata mimba.

Moja ya tatizo alilokutwa nalo amesema na homoni kutokuwa sawa na baada ya kutumia dawa ndio akapata mimba.

Kwa upande wake mtaalam wa masuala ya uzazi,Hosiana Sanga kutoka kampuni bidhaa za virutubisho vya uzazi, ,amesema amekuwa akipokea simu nyingi za matatizo ya uzazi na sasa yameenda mbali zaidi hadi kwa wanaume.

Anataja moja ya tatizo la masuala ya uzazi kwa wanaume ni pamoja na ulaji mbaya ikiwemo kula chipi mayai.