Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Albamu ya Kendrick Lamar moto wa kuotea mbali

Kendrick Pict
Kendrick Pict

Muktasari:

  • Albamu hiyo iliyoachiwa Novemba 22, iko mbioni kuweka rekodi kama albamu ya Hip Hop iliyosikilizwa zaidi (most streamed) kwa mwaka huu katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali ya kusikiliza muziki duniani.

Rapa wa Marekani, Kendrick Lamar, 37, anaendelea kuonyesha ubabe wake katika ulimwengu wa Hip Hop kufuatia mapokezi  makubwa ya albamu yake ya sita, GNX (2024) ambayo imetoka hivi karibuni kwa kushtukiza.

Albamu hiyo iliyoachiwa Novemba 22, iko mbioni kuweka rekodi kama albamu ya Hip Hop iliyosikilizwa zaidi (most streamed) kwa mwaka huu katika majukwaa mbalimbali ya kidijitali ya kusikiliza muziki duniani.

Mradi huo uliotoka chini ya PGLang na Interscope Records umeshirikisha wasanii kama AzChike, Dody6, Hitta J3, Peysoh, Roddy Ricch, Siete7x, SZA, Wallie the Sensei, YoungThreat, Deyra Barrera, Sam Dew, Ink n.k.

Hii ni albamu ya kwanza ya Lamar kutoa tangu kuachana na lebo mbili za Top Dawg Entertainment na Aftermath Entertainment ambazo alifanya nazo kazi kwa miaka mingi.

Rapa huyo alitambulika zaidi kupitia albamu yake ya pili, Good Kid, M.A.A.D City (2012) ikiwa ni baada ya kurekodi na Dr. Dre chini ya Aftermath Entertainment, lebo iliyowakuza wakali wengine kama Busta Rhymes, Snoop Dogg, 50 Cent, Eminem n.k.

Kwa mujibu wa Top Of The Charts, inakadiriwa kuwa ndani ya wiki moja albamu hiyo mpya ya Kendrick Lamar, GNX (2024) ilisikilizwa (streams) mtandaoni kati ya mara milioni 350 hadi 400.

Hii inaifanya kuwa albamu ya Hip Hop iliyosikilizwa zaidi ndani ya wiki moja kwa mwaka huu, sawa na ile ya Drake, For All the Dogs (2023) ambayo ilisikilizwa mara milioni 514 pindi ilipotoka mnamo Oktoba 6, 2023.

Ikiwa albamu hiyo itaendelea kwa mwendo huo, GNX haitaonyesha tu kukubalika kwa Lamar kwenye tasnia ya muziki duniani, bali pia itaimarisha uwezo wake wa kufikia mafanikio muhimu ya kibiashara katika mfumo ambao unakubadilika.

Lamar ambaye pia ni mtayarishaji mkuu wa albamu hiyo kwa kushirikiana na Dave Free, inasemekana kuwa anajiandaa kufanya ziara ya dunia (world tour) baada ya onyesho lake la Super Bowl Halftime mapema mwakani.

Hayo yanajiri mwezi mmoja baada ya Lamar kushinda tuzo nane za BET Hip Hop 2024 akiwa ndiye msanii aliyefanya vizuri zaidi, huku wimbo wake maarufu kwa sasa, Not Like Us (2024) ukishinda vipengele vitatu.

Albamu iliyopita ya Lamar, Mr. Morale & The Big Steppers (2022) ilifanya vizuri ikishaka namba moja chati ya Billboard 200 huku akishinda katika tuzo za 65 za Grammy kama Albamu Bora ya Rap na kwa ujumla iliteuliwa katika vipengele nane.

Lamar akizungumza na jarida la W Magazine hapo Oktoba 2022, alisema watoto wake walichangia kwa sehemu katika uandaaji wa albamu hiyo na kikubwa ilimfunza namna ya kujishusha zaidi maishani mwake.

Ikumbukwe rapa huyo ametumia sauti za familia yake katika nyimbo zake mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na zile za mama na baba yake mzazi.

Vilevile sauti ya mchumba wake  Whitney Alford imesikika katika nyimbo zake nne, miongoni mwa hizo ni Mother I Sober (2022) na Father Time (2022).

Wawili hao walikutana kama wanafunzi wa shule ya sekondari ya Centennial katika mji wao wa nyumbani huko Compton, California, kusini mwa Los Angeles, walikuwa marafiki kwanza kabla ya kuwa wapenzi na walionekana hadharani kwa mara ya kwanza mwaka 2014.