Daimond na warembo hawa ipi kali zaidi?
SUPASTAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekuwa kioo cha chipukizi wanaoingia kwenye muziki kutoaka na aina ya maisha yake yanayoonekana mbele ya jamii.
Ni tajiri wa nyimbo, lakini Mwanaspoti linakuchambulia zile alizoimba na wazazi wenzake ama warembo anahusishwa kutoka nao kimapenzi.
Katika nyimbo hizo alizoimba na warembo hao je ni ipi kali na kupendwa zaidi na mashabiki?
MTASUBIRI
Wimbo wa Mtasubiri ndio unaotamba kwa sasa Diamond Platnumza ameimba na msanii anayemsimamia Zuchu, jambo linalowafanya mashabiki wahisi wawili hao huenda ni wapenzi, kutokana na maisha wanayoyaonyesha mbele ya mashabiki wao.
SALOME
Wimbo wake wa Salome, Diamond Platnumz alimtumia Hamasa Mobeto kama video Queen, ambaye baadae akapata naye mtoto anayejulikana kwa jina la Deedaylan, nyakati hizo wimbo huo ulitamba kila kona.
GERE
Wimbo wa Gere Diamond Platnumz alishirikishwa na mzazi mwenzake Tanasha Donna aliyezaa naye mtoto anaitwa Naseeb Jr, wakati wapo mapenzi wimbo wao ulikuwa unatamba zaidi.
UTANIPENDA
Wakati wimbo wa 'Utanipenda' ulipendwa na kuimbwa kila kona, ndani ya mashairi alimtaja binti yake Latifah 'Tifah' mzazi mwenzake Zari The Boss Lady na mama yake mzazi.
Ni wimbo uliomhusu zaidi, kutokana na kuizungumzia familia yake na watu wanaomzunguka, Diamond Platnumza amezaa watoto wawili za Zari The Boss Lady ambao ni Tifah na Nillan.