Mourinho kumpumzisha Pogba

Muktasari:

  • Mourinho amesema hiyo inatokana na idadi kubwa ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kuwa na uchovu baada ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.

Moscow, Russia. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, amesema hafurahii mwanzo wa msimu mpya wa Ligi kuu England.

Mourinho amesema hiyo inatokana na idadi kubwa ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kuwa na uchovu baada ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.

Alisema wachezaji walioshiriki fainali za Kombe la Dunia wamechoka na wanahitajika kupumzika na yeye kwa kutambua hilo amepanga kutowatumia katika mechi za kwanza za msimu mpya wa Ligi.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na Inter Milan, alisema kuna muda mfupi wa mapumziko kwa wachezaji hao kabla ya kuanza kwa Ligi hivyo anahisi akiwatumia atakua kama anayecheza Kamari itakayomgharimu baadaye.

“Sitawatumia wachezaji walioshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu katika mechi za kwanza za Ligi kuu, tunahitaji wapumzike na kurudisha nguvu za ushindani,” alisema.

Wachezaji wa United walioshiriki fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia ni, Paul Pogba (Ufaransa), Nemanja Matic (Serbia), Marcus Rashford, Jesse Lingard (England), Marouane Fellaini (Ubelgiji) na kipa David De Gea (Hispania).