#WC2018: Jamaa wametoboa bila kwenda shule

Muktasari:

  • Lakini, kufikia ndoto za kucheza fainali za Kombe la Dunia hazihitaji kwenda shule, kwani kuna mastaa mahiri hao duniani, hawajawahi kwenda shule, lakini wamefanikiwa kucheza kwenye fainali za Kombe la Dunia, baadhi yao zikiwamo fainali za mwaka huu zilizomalizika jana Jumapili huko Russia kwa mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Croatia.

KOMBE la Dunia ndio fainali za soka ambazo kila mwanasoka duniani anakuwa na ndoto ya kwenda kucheza siku moja. Wapo waliofanikiwa kutimiza ndoto hizo za kucheza kwenye fainali za soka za Kombe la Dunia na wapo ambao wamefeli.

Lakini, kufikia ndoto za kucheza fainali za Kombe la Dunia hazihitaji kwenda shule, kwani kuna mastaa mahiri hao duniani, hawajawahi kwenda shule, lakini wamefanikiwa kucheza kwenye fainali za Kombe la Dunia, baadhi yao zikiwamo fainali za mwaka huu zilizomalizika jana Jumapili huko Russia kwa mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Croatia.

5. Ronaldinho

Ronaldo de Assis Moreira, maarufu zaidi kwa jina la Ronaldinho, alichagua soka mbele ya shule.

Kipaji chake cha soka kilianza kuonekana akiwa na umri wa miaka minane tu na hapo ndipo alipopachikwa jina la “Ronaldinho” kwa sababu alikuwa mchezaji mdogo zaidi katika mechi za timu za watoto. Aliendelea kucheza kwenye futsal na soka la ufukweni na baadaye akaweka mkazo kwenye soka ambalo lilimfanya kuwa maarufu zaidi duniani. Alikuwa gumzo akiwa na umri wa miaka 13 ambapo kwenye mechi moja ambayo timu yake ilishinda 23-0, mabao yote siku hiyo alifunga yeye.

4. Didier Drogba

Drogba alizaliwa Abidjan, Ivory Coast na akiwa na umri wa miaka mitano alihamia Ufaransa na wazazi wake kwenda kuishi kwa mjomba wake, Michel Goba, aliyekuwa mwanasoka. Lakini ghafla

Drogba akakumbuka nyumbani, hivyo akarudi Abidjan baada ya miaka mitatu tu. Lakini, wazazi wake wote wawili wakapoteza kazi zao, hivyo Drogba ilibidi arudi tena kwa mjomba wake. Hakupata nafasi ya kwenda shule, hivyo akajiunga moja kwa moja kwenye klabu ya Levallois.

3.Cristiano Ronaldo

Kwa upande wa Ronaldo, soka ndiyo ilikuwa shule yake na mechi kubwa ndiyo ilikuwa mitihani yake. Akiwa mtoto mdogo, Ronaldo alicheza soka la ridhaa kwenye timu ya Andorinha kuanzia 1992 hadi 1995.

Baba yake alikuwa mtunza vifaa wa timu hiyo na miaka miwili baadaye akaenda kuichezea Nacional. Mwaka 1997, akiwa na umri wa miaka 12, alikwenda kufanya majaribio kwa siku tatu kwenye klabu ya Sporting CP, ambayo ilimsainisha kwa ada ya Pauni 1,500. Alijaribu kuwa mwanafunzi wa shule, lakini alifukuzwa baada ya kumrushia kiti mwalimu.

2. Lionel Messi

Messi alijiunga na Rosario wakati akiwa na umri wa miaka sita. Kwa miaka hiyo sita aliichezea Newell’s, alionyesha kiwango bora kabisa na kutengeneza kumbukumbu ya kipekee kwenye timu hiyo. Baada ya mwaka mmoja kwenye akademia ya Barc elona, La Masia, Messi akaoro dheshwa kwenye Shirikisho la soka la Hispania (RFEF) Februari, 2002.

Baada ya kuka milisha tiba yake ya kutibiwa homoni za kumfanya akue kipindi akiwa na umri wa miaka 14, Messi aka weka rasmi kwenye kikosi cha timu ya Ba rcelona huko La Masia na sasa kuwa mchezaji mashuhuri kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Nou Camp.

1. Neymar

Neymar alichanganya mapenzi yake ya futsal na soka la mitaani. Mwaka 2003, Neymar alihamia na familia yake Sao Vicente, ambako alikwenda kuichezea timu ya watoto ya Portuguesa Santista. Mwaka huohuo, alihamia Santos, ambako Neymar alikwenda kujiunga na Santos FC.

Kutokana na mafanikio yake, akisaidia kipato cha nyumbani na familia yake kuanza kununua nyumba jirani na Vila Belmiro. Familia yake ikawa vizuri baada ya Neymar kufikisha umri wa miaka 15, alikuwa akilipwa pesa nyingi. Akiwa na umri wake 17, alisaini mkataba wa kwanza kuchezea kikosi cha kwanza cha Santos na hapo akaanza kusaini dili tamutamu za kibiashara na sasa ni bonge la tajiri.