#WC2018: Philipp Lahm, Natalia Vodianova kupeleka Kombe Luzhniki

Friday July 13 2018

 

Moscow, Russia. Jumapili, Julai 15 mwaka huu, macho na masikio ya mashabiki wa soka, yataelekezwa katika uwanja wa Luzhniki, wenye uwezo wa kuhukua mashabiki 81,000 kwa ajili ya kushuhudia mtanange wa kukata na shoka wa fainali ya Kombe la Dunia 2018, kati ya Ufaransa na Croatia.
Mechi hii itatimua vumbi kuanzia saa 12 jioni ambapo ulinwengu wa soka utashuhudia moja kati ya mambo mawili, Croatia wakilipiza kisasi cba mwaka 1998 au Ufaransa kutwa kombe lao la pili. Kitu kingine ambacho kinaweza kutokea ni Ufaransa kuendeleza ubabe wao dhidi ya watoto wa mama.
Sasa kabla ya mtanange huo, ulimwengu wa soka utamkaribisha nahodha wa zamani wa Ujerumani, Philipp Lahm akiongozana na Mlimbwende wa Kirusi, Natalia Vodianova. Wawili hao wataenda Luzhniki kwa ajili ya kazi moja; kupeleka mwali.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na FIFA, Lahm ambaye aliiongoza Ujerumani kutwaa taji hilo, pamoja na Vodianova, watapeleka kombe hilo, ukiwa umehifadhiwa katika kisanduku maalum, uliotengezwa na mtaalam, Louis Vuitton.
Kombe hilo, maarufu kama Jules Rimet, lenye urefu wa sentimeta 36, uzito wa kilo 6.175 na ambayo imeundwa na dhahabu,
litakabidhiwa kwa mshindi kati ya Ufaransa na Croatia ambapo tayari mwamuzi, Nestor Pitana, kutoka Argentina ameteuliwa kupuliza kipyenga, akisaidiwa na Hernan Maidana na Juan Belatti.