STRAIKA WA MWANASPOTI : Wakongwe kurudi dimbani, inasaidia kuinua soka

Muktasari:

  • Nikikupa tu historia fupi kuhusu ligi hiyo ambayo ilianzishwa miaka minne iliyopita.

LIGI Kuu ya wachezaji waliostaafu nchini Kenya msimu wa nne ilifikia kikomo juzi Jumapili Jijini Kisii baada ya Tusker Wazee FC kushinda taji hilo kwa mara ya pili.

Nikikupa tu historia fupi kuhusu ligi hiyo ambayo ilianzishwa miaka minne iliyopita.

Ni lazima uwe umestaafu na uko na zaidi ya miaka 35. Mara ya kwanza ligi hii ilianzia jijini Eldoret wakati timu ya wazee wa Tusker, Eldoret Mambuyu na Luo Odich ya Kisumu zilipokutana. Tusker iliibuka washindi. hio ulikuwa mwaka wa 2015.

Msimu uliofata kulikuwa timu kadhaa zikijiunga zikiwemo Leysa, Bandari ya Mombasa, Naivasha, USIU na Nakuru Wazee.

Leysa waliibuka washindi msimu wa 2016. Msimu wa 2017 Timu Kama, MTRH ya Eldoret, Kibra Wazee, Maseno Paradiso, Kisii Wazee, Machakos Maveto, Kenyatta Hospital wakaingia pia Wait.

Ni msimu ambao Leysa walinyakua taji hilo kwa Mara ya pili mfululizo. Tusker Wazee msimu huu wakajipanga vyema na kwa kweli haikuwa kubahatisha wakati waliponyakua taji hilo msimu huu 2018.

Haswa madhumuni ya ligi hii ni kuwaleta wachezaji waliostaafu pamoja na kujua vile watu wanaweza saidia. Imechangia kufahamu wachezaji wetu wako Wapi. Kitu ambacho hufanyika, hizo timu zote 14 hujikusanya katika jiji moja na kuchagua sehemu ambayo ipo na zaidi ya viwanja vitatu.

Kwa siku kila klabu hucheza mechi mbili. Ni mechi ambazo zimesaidia kuweka wachezaji waliostaafu pamoja na kujua kila mtu anafanya kazi gani baada ya kustaafu. Kwa kizungu inaitwa Net Working.

Ni ligi ambayo ipo na wachezaji tajika. Ukiangalia katika kikosi cha Tusker kunao wachezaji Kama Sammy Pamzo Omollo ambaye ni Kocha wa Posta Rangers.

Kunaye Titus Mulama, Zablon Amanaka, Godwin Odinde, Fred Ambani, Bonface Ambani, na kadhalika, ukitazama Bandari kunao Jamal, Father na Evans Orodi waliokuwa wakichezea Bandari zama zile.

Eldoret Mambuyu kunao akina Charles Odero, na Francis Baraza, Ukienda Naivasha kunaye Nichola Muyoti ambaye ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Nzoia FC, Leysa kunao wachezaji Kama, Oscar Kadenge na Pablo wote wachezaji tajika.

Ukiangalia kikosi cha Kibra UTD kunao wachezaji kama, Paul Ochieng na Deo wachezaji walisakata soka katika Klabu ya AFC Leopards.

Kwa hivyo jambo ambalo la muhimu hapa limekuwa ni kuunganisha wachezaji kwa pamoja. Ukiangalia utapata kwa mfano wakati mchezaji anapopata shida, kuitatua inakuwa ni haraka kwa upande wao.

Hata hangaika pekee yake. Kwa mfano kuna mmoja wetu aliaga dunia kwa ajali ya barabarani timu zote zilijitolea na kuhakikisha amesaidika vilivyo.

Familia yake haikutoa hata senti moja. Na sio hivyo pekee. Ligi hii imesaidia wachezaji kadhaa wameandikwa kazi hapa na pale.

Kwa hivyo ndugu zanguni saa hizi tunatazamia kuhakikisha klabu zote zifike 20 kabla ya 2020. Ni Muhimu sana na natarajia mda sio mrefu saana itakuwa imepata wadhamini.

Natumai kuona wenzetu Tanzania, Uganda, Rwanda na kadhalika wakianzisha hizi ligi ya namna hii.

Kwa sababu zitasaidia kuimarisha na kuboresha maisha yetu haswa wachezaji waliostaafu. Pia kama nilivyo sema hapo awali wachezaji wengi hapa ni makocha na wao pia huzunguka wakitafuta vipaji nchini kote. Ni ligi ambayo iko na mitazamo yake pia. Nilazima uwe zaidi ya miaka 35 na usiwe unacheza ligiiyeyote nchini.

Hongera Tusker Wazee na Kocha wa Njuguna ambaye enzi zake alikuwa mchezaji wa Klabu ya Tusker mmeonyesha kazi nzuri kwa muda wote katika ligi na sasa imebaki kuwa heshima kwetu.

Msimu ujao ligi inaanzia Mombasa. Bandari wataandaa mashindano hayo kabla Maseno Paradiso waandae mashindano hayo mwezi wa nane.