STRAIKA WA MWANASPOTI : Liverpool izidi kukaza kamba pale England

Tuesday January 21 2020

Liverpool izidi kukaza kamba pale England-Manchester United-Ligi Kuu England-Man City

 

By Boniface Ambani,Nairobi

USHINDI wa Liverpool dhidi ya Manchester United, juzi Jumapili ulikuwa ni hakikisho dhabiti kwamba vijana wa Anfield msimu huu Ligi Kuu England umedhihirisha ubingwa ni wao.

Ikumbukwe kabla ya kuifunga Man United, Liverpool ilitoka kuifunga Tottenham kwa bao 1-0. Tottenham iko chini ya kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho.

Ushindi huo wa Kocha Jurgen Kloop dhidi ya Ole Gunnar Soljsker ilikuwa ni barua kwa dunia nzima kwamba huu msimu anaingia historia kama kocha wa kwanza kunyakua taji hilo tangu Ligi Kuu ibadilishwe jina. Kloop amejiandikishia historia ambayo itachukua mda kufutika.

Lakini Jambo ambalo niwatahadharisha ni kwamba ligi bado changa hasa ikikumbukwa ni nani anaye wafata hapo mgongoni mwao.

Liverpool inaongoza jedwali hilo ikiwa na alama 64 ikifuatiwa kwa karibu kidogo na mabingwa watetezi Man City wakiwa na alama 48.

Hizo no alama 16 tu.T ukumbuke kwamba mzunguko wa pili, ndio umeng’oa nanga hivi karibuni. Inamaanisha bado Liverpool iko na mechi 16 za kupigania Ligi Kuu hiyo. Isije ikateleza. Nakumbuka miaka za hapo awali Arsenali iliongoza jedwali na zaidi ya alama 14. Lakini Manchester United ilifukuzana nayo na baada ya mwisho wa msimu Man United ilitawazwa kuwa mabingwa. Jambo ambalo naweza kulisema kwamba limesaidia Liverpool msimu huu ni kwanza.

Advertisement

Kwanza Kloop hakununua wachezaji wowote wa kuwaingiza kwenye kikosi cha kwanza. Amemchukua Takumi Minomono kutoka Sulzubrg ya Austria.

Mchezaji huyo ataingia kwenye mfumo taratibu wakati kina Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino watakapokuwa wamechoka. Alikuwa na kikosi hatari ambacho kilimshindia klabu bingwa barani Ulaya. Kikosi hicho hicho kikamaliza msimu wa Ligi Kuu katika nafasi ya pili msimu ulioisha.

Kloop hakununua wachezaji. Aliuza tu na wengine akawapeleka kwa mkopo. Pili, kikosi cha Kloop hakijakuwa na majeraha mengi.

Wamewaza kujiweka katika nafasi nzuri saana ya kiafya. Majeraha hayajawasumbua hata kidogo. Pia, tangu msimu uanze haijapoteza mechi yeyote. Ni Jambo la muhimu sana. Jambo lingine la maana sana ni kwamba imeweza kupata alama tatu kutoka kwa wapinzani wao wakaribu sana.

Ukiangalia kwa karibu na kwa undani zaidi, hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yameweza kusaidia klabu hiyo kufika sehemu ilipo sasa hivi.

Hata hivyo, mzunguko wa pili umeanza. Lazima iichunge Manchester City vilivyo. Ikiteleza tu inaweza kufanya mambo yake. Bahati mbaya kwa upande wake juzi Man City ilitoka sare na Cryastal Palace ya mabao 2-2. Hiyo ilikuwa ni afueni kwa Liverpool ambayo sasa imeweza kupanua tofauti ya pointi kufikia 16.

Hiyo inaonyesha Kloop anafaa kuzidi kutanua tofauti hiyo ya magoli kwasababu Man City ina mabao mengi zaidi yake.

Liverpool ipo na magoli 52 ya kufunga. Man City ina magoli 64. Ina maana lazima Liverpool ijichunge sana kwenye pointi kwa kuhakikisha inaiacha timu hiyo inayonolewa na Pep Guardiola kwa pointi nyingi. Iwapo itateleza, Man City itawapita kwa mabao mengi kama alama zitakuwa sawa.

Hivyo kutakuwa na kazi ya kufanya upande wa kuhesabu magoli. Kwa hivyo Liverpool jambo inalotakiwa kulifanya ni kuongeza pia idadi ya mabao. Lolote linaweza tokea.

Hata hivyo, mziki bado unaendelea. mechi nane zifuatazo za Liverpool zitatupa habari kamili ya mwelekeo wa ligi hiyo.

Hayo yakijiri, mbio bado zipo klabu nyingine nne ambazo zinatafuta nafasi ya kumaliza nne bora.

Klabu hizo za Man City, Leicester City, Chelseana Man United ni baadhi tu ya klabu ambazo zinafukuzana na angalau kumaliza ndani ya nne bora.

Lengo la klabu hizo ni kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa Man City hakuna shida ina uhakika kama itashindwa kuishusha Liverpool kwenye mbio za ubingwa, basi itaweza kujikatia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Advertisement