WALETE: Kila mbabe na mbabe wake robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

NYON, USWISI,

KWANI kuna habari gani. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wote wametinga kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Paul Pogba, Sergio Aguero, Harry Kane na Mohamed Salah ni wakali wengine waliotinga na timu zao kwenye hatua hiyo ya kibabe kabisa huko kwenye michuano ya Ulaya.

Kile kitendawili cha nani atacheza na nani, kitateguliwa leo Ijumaa huko mjini Nyon, Uswisi.

Vigogo nane waliotinga hatua hiyo ni Ajax, FC Porto, Manchester United, Manchester City, Juventus, Liverpool, Tottenham Hotspur na Barcelona. Kwenye hatua hiyo ya robo fainali, yeyote anayeweza kupangwa na yeyote. Ile mara paap, Ronaldo dhidi ya Messi.

Wakati ukisubiri kuona hiyo droo itakavyopangwa kutambua nani atacheza na nani, hivi unajua rekodi za timu zote nane zilizofika hatua hiyo zipoje kwenye mechi walizokutana wenyewe kwa wenyewe.

Cheki hapa rekodi ya kila timu zilizofika robo fainali katika mechi walizokutana wenyewe kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ajax

(Uholanzi)

Msimu huu imeshinda mechi nane, sare tano, imepoteza moja, mabao ya kufunga 29 na kufungwa 12. Dusan Tadic, aliyefunga mabao tisa yakiwa matatu katika mechi za kufuzu, ndiye kinara wao wa mabao hadi sasa.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Barcelona - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 3, kufungwa 10

v Juventus - wameshinda 2, sare 4, kuchapwa 6, mabao ya kufunga 9, kufungwa 15

v Liverpool - wameshinda 1, sare 1, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 7, kufungwa 3

v Man City - wameshinda 1, sare 1, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 5, kufungwa 3

v Man United - wameshinda 2, sare 0, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 3, kufungwa 7

v Porto - wameshinda 1, sare 1, kuchapwa 4, mabao ya kufunga 2, kufungwa 8

v Tottenham - wameshinda 0, sare 0, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 1, kufungwa 6

Barcelona

(Hispania)

Rekodi zao za msimu huu, wameshinda mechi tano, sare tatu, haijapoteza, mabao ya kufunga 19 na kufungwa sita. Kinara wao wa mabao ni Lionel Messi aliyetikisa nyavu mara nane.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 3, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 10, kufungwa 3

v Juventus - wameshinda 4, sare 4, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 13, kufungwa 10

v Liverpool - wameshinda 2, sare 3, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 6, kufungwa 6

v Man City - wameshinda 5, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 12, kufungwa 5

v Man United - wameshinda 4, sare 4, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 20, kufungwa 15

v Porto - wameshinda 5, sare 0, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 15, kufungwa 9

v Tottenham - wameshinda 2, sare 2, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 7, kufungwa 4

Juventus

(Italia)

Kwenye mchakamchaka huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, Juventus imeshinda mechi tano, sare hakuna, wamepoteza tatu, mabao ya kufunga 12 na wamefungwa sita. Anayeoongoza kwa mabao kwenye kikosi chao ni Paulo Dybala, aliyeweka kwenye kamba mara tano.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 6, sare 4, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 15, kufungwa 9

v Barcelona - wameshinda 3, sare 4, kuchapwa 4, mabao ya kufunga 10, kufungwa 13

v Liverpool - wameshinda 3, sare 1, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 5, kufungwa 4

v Man City - wameshinda 3, sare 2, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 7, kufungwa 4

v Man United - wameshinda 6, sare 2, kuchapwa 6, mabao ya kufunga 17, kufungwa 17

v Porto - wameshinda 4, sare 1, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 8, kufungwa 2

v Tottenham - wameshinda 1, sare 1, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 4, kufungwa 3

Liverpool

(England)

Msimu huu wameshinda mara nne, sare moja na wamechapwa mara tatu, huku wakifunga mabao 12 na kufungwa manane. Masupastaa Sadio Mane na Mohamed Salah ndio waliofunga mara nyingi kwenye timu hiyo kila mmoja akifunga mara tatu.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 3, kufungwa 7

v Barcelona - wameshinda 3, sare 3, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 6, kufungwa 6

v Juventus - wameshinda 2, sare 1, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 4, kufungwa 5

v Man City - wameshinda 2, sare 0, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 5, kufungwa 1

v Man United - wameshinda 1, sare 1, kufungwa 0, mabao ya kufunga 3, kufungwa1

v Porto - wameshinda 3, sare 3, kufungwa 0, mabao ya kufunga 12, kufungwa 2

v Tottenham - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 2, kufungwa 2

Manchester City

(England)

Kocha Pep Guardiola na kikosi chake cha Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu ameshinda mechi sita, sare moja, kuchapwa moja, mabao ya kufunga 26 na kufungwa manane tu. Straika, Sergio Aguero ndiye mfungaji kinara kwenye kikosi hicho akifunga mara tano.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 3, kufungwa 5

v Barcelona - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 5, mabao ya kufunga 5, kufungwa 12

v Juventus - wameshinda 1, sare 2, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 4, kufungwa 7

v Liverpool - wameshinda 0, sare 0, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 1, kufungwa 5

v Man United - hazijawahi kumenyana

v Porto - wameshinda 2, sare 0, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 6, kufungwa 1

v Tottenham - hazijawahi kukutana

Manchester United

(England)

Wababe wa Old Trafford, Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya walifanya maajabu kwa kuwatupa nje PSG. Rekodi zao za msimu huu wameshinda mara nne, sare mona na wamechapwa tatu, mabao ya kufunga 10 na wamefunga saba. Kinara wao wa mabao ni Romelu Lukaku, Paul Pogba, na Marcus Rashford, ambao kila mmoja amefunga mara mbili.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 3, sare 0, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 7, kufungwa 3

v Barcelona - wameshinda 3, sare 4, kuchapwa 4, mabao ya kufunga 15, kufungwa 20

v Juventus - wameshinda 6, sare 2, kuchapwa 6, mabao ya kufunga 17, kufungwa 17

v Liverpool - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 1, kufungwa 3

v Man City - hazijawahi kumenyana

v Porto - wameshinda 3, sare 3, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 14, kufungwa 11

v Tottenham - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 4, kufungwa 3

FC Porto

(Ureno)

Wareno FC Porto wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu huko kwenye michuano ya Ulaya, wakishinda mechi sita, sare moja, kichapo kimoja mabao ya kufunga 19 na wamefungwa tisa tu. Kinara wao wa mabao ni Moussa Marega, aliyetupia nyavuni mara sita.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 4, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 8, kufungwa 2

v Barcelona - wameshinda 3, sare 0, kuchapwa 5, mabao ya kufunga 9, kufungwa 15

v Juventus - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 4, mabao ya kufunga 2, kufungwa 8

v Liverpool - wameshinda 0, sare 3, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 2, kufungwa 12

v Man City - wameshinda 0, sare 0, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 1, kufungwa 6

v Man United - wameshinda 2, sare 3, kuchapwa 3, mabao ya kufunga 11, kufungwa 14

v Tottenham - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 1, kufungwa 3

Tottenham Hotspur

(England)

Tottenham Hotspur kwenye rekodi zao za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wameshinda mechi nne, sare mbili, vichapo viwili huku wakiwa na mabao ya kufunga 13 na kufungwa 10. Supastaa Mwingereza, Harry Kane ndiye kinara wao wa mabao aliyetupia nyavuni mara tano.

Rekodi zao dhidi ya timu nyingine zilizotinga robo fainali

v Ajax - wameshinda 2, sare 0, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 6, kufungwa 1

v Barcelona - wameshinda 0, sare 2, kuchapwa 2, mabao ya kufunga 4, kufungwa 7

v Juventus - wameshinda 0, sare 1, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 3, kufungwa 4

v Liverpool - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 2, kufungwa 2

v Man City - hazijawahi kukutana

v Man United - wameshinda 1, sare 0, kuchapwa 1, mabao ya kufunga 3, kufungwa 4

v Porto - wameshinda 1, sare 1, kuchapwa 0, mabao ya kufunga 3, kufungwa 1.