Hongera Simba, Gor Mahia mlipofikia jipangeni sasa

Muktasari:

  • Tatizo lililojitokeza lilikuwa ulinzi wa Simba ulionekana kufifia kabisa. Jambo ambalo klabu ya Simba inafaa kulifanyia kazi.

Safari ya Simba Sports Club kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilifikia kikomo baada ya kupigwa kichapo Cha mabao 4-1 na TP Mazembe ya Congo siku ya Jumamosi.

Ni mechi ambayo Simba waliianza vizuri kabisa kwa Emmanuel Okwi kupachika bao la mapema sana.

Simba walionekana wangeweza kushikilia lakini kwa kweli waliachilia ushindi ambao ungewapeleka katika nusu fainali.

Tatizo lililojitokeza lilikuwa ulinzi wa Simba ulionekana kufifia kabisa. Jambo ambalo klabu ya Simba inafaa kulifanyia kazi.

Simba viungo wapo, washambuliaji wapo lakini walinzi ndio tatizo.

Mabeki wao haswaa hawako katika viwango ambavyo unastahili. Waliingia mchecheto na hatimaye wakasalimu amri. Hata hivyo, nawapongeza kwa kupiga hatua ya kuingia robo fainali. Inafaa Sasa washikilie hapo msimu ujao pia wafanye bidii waingie robo fainali.

Makosa naweza kusema tu ni kwamba Simba hawakutumia nafasi zao nyumbani kwao Dar. Ni lazima wakati wowote ule unapocheza nyumbani kwenu utumie fursa hiyo kujitetea na kujieleza vizuri. Ndio njia hiyo tunajifunza.

Wakati hali ikiwa hiyo kwa Simba, Gor Mahia ilitandikwa mabao 5-1 na RS Berkane ya Morocco siku ya Jumapili. Ilikuwa shughuli kubwa pale Morocco. Ukumbuke kuwa mechi ya kwanza hapa Gor Mahia ilikuwa ishaa poteza mechi hiyo kwa kukubali kichapo cha mabao 2-0 jijini Nairobi.

Ninarudi pale pale kwa Simba. Ni lazima utumie Uwanja wako wa nyumbani vilivyo. Masaibu ya Gor Mahia yalikumbwa na usafiri. Usafiri ambao umeleta tumbo joto nchini Kenya.

Ndugu zanguni kwa upande wangu kama mdadisi wa maswala ya soka. Klabu ya Gor Mahia walijidunga msumari punde tuu walipokubali kucheza mechi ya dhidi ya Bandari siku ya jumatano.

Hiyo ni mechi ambayo ingetolewa, ili iwape muda mwafaka wa kusafiri. Kitumbua kiliingia mchanga punde tu walikubali hiyo mechi ya Bandari. Usafiri kwa kuelekea Morocco, Algeria, Tunisia huwa na shida saana.

Hakuna ndege ya moja kwa moja. Kutoka Kanda hili letu kwenda nchi hizo. Unahitaji kusafiri kupitia nchii kadha wa kadha kabla ufike hizo nchi.

Itakuchukua saa kadhaa kusafiri. Kwa hivyo lazima utoke mapema. Ni safari iliyokumbwa na misukosuko na hatimaye matokeo ndio hayo. Mimi kwangu husema ni dunia tuu hufunza walimwengu.

Wamejifunza na hawatarudia makosa kama hayo siku nyingine. Gor Mahia wamebanduliwa,Simba Sports club nje pia. Ni kujipanga Sasa.

Wakati huo huo cha kufurahisha ni kwamba droo ya Kuwania kombe la mataifa barani ulaya ilifanyika nchini Misri juzi. Kenya,Tanzania,Senegal na Algeria zimepangwa katika kundi la C. Kazi ipo.

Kwa hivyo matayarisho lazima yawe yameshaaanza. Isifike wiki ya mwisho ndipo mnaanza kukimbizana hapa na pale. La hasha. Matayarisho lazima yaanze Leo Leo.

Nikiangalia Harambee Stars naona wanaelekea kupiga kambi yao rasmi ufaransa na Kuna matumaini makubwa kuwa wataeza kupiga mechi ya kurafiki kwa mara ya kwanza na timu ya Taifa ya Ufaransa. Angalau naona matayarisho yameanza.

Na ni lazima pia Serikali zetu zijiunge na kusaidia matayarisho hayo. Tusifike Misri tuwe watu wa kusindikizana. Hapana. Lazima tupige hatua kutoka katika makundi.

Kanda hili la Afrika Mashariki na ya kati tumewakilushwa vilivyo. Hamna sababu ya sote kurudi nyumbani malema.

Kenya, Tanzania, Uganda,na Burundi sisi wote hao tunaelekea Misri. Ni lazima tujitahidi. Ni kuwatakia kila la kheri katika matayarisho hayo. Kwa Gor Mahia na Simba sisi husema tumerudi ubaoni kuchora mikakati. Tumejua upungufu wetu uko wapi. Ni kupiga huo upungufu msasa. Siku njema.