Tumia mbinu hizi za kujipodoa uonekane mrembo

Tuesday July 3 2018

 

Mara nyingi kiwango cha urembo hutegemea na jinsi ulivyojipaka vipodozi vyako. Mbinu hizi za kujipodoa zitakusaidia uonekane maridadi.

·Songea karibu na kioo iwezekanavyo, inua kichwa chako huku ukiweka kidevu chako karibu sana na kioo. Hii itakusaidia kuona sehemu zingine za uso vizuri unavyoendelea kujipaka.

·Tumia brashi maalumu kupaka foundation ikiwa unataka sehemu zote kuonekana sawa na iwapo unataka mapambo yako yaonekane kama yameenea kwa viwango sawa.

·Kila mara paka penseli ya hudhurungi kwenye sehemu ya juu ya nyusi ili kufanya uso wako uonekane kama umeinuka.

·Unapojipaka vipodozi anza kwa kupaka rangi hafifu kabla ya kuongeza rangi inayoandamana na rangi yako halisi hasa ikiwa uso wako una sehemu zenye rangi tofauti.

·Kila mara paka poda zaidi katika sehemu za uso zinazoonekana kung’aa sana ikilinganishwa na sehemu zingine.

Advertisement

·Unapaswa kutumia bronzer kwenye shingo, uso na kifua chako kusawazisha rangi ya ngozi yako sehemu zote.

·Unapopaka blush kwanza tabasamu kisha uanze kupaka ukielekea upande wa juu wa sikio kisha ukielekea kwenye utaya. Hii itahakikisha mapambo yameenea vizuri hata unapotabasamu au kucheka.

·Unapojipaka mascara fanya hivyo kwa utaratibu huku ukipanguza brashi yake kwenye karatasi shashi kuondoa rangi zaidi.

Advertisement