GAUNI Wewe unalivaaje? Chukua maujanja hapa

Thursday April 19 2018

 

By ELIZABETH TUNGARAZA

MARA nyingi wanawake wanaofanya kazi hupata changamoto wakati wa kutafuta nguo za kuvaa asubuhi wakijiandaa kwenda kazini.

Basi leo tuangalie jinsi gauni linavyoweza kukupa mwonekano mzuri kazini kwako.

Tafuta gauni simpo ambalo unaweza kulistyle vyovyote vile upendavyo. Cha msingi tafuta gauni ambalo linaendana na umbo lako ili kupata mwonekano mzuri mbele za macho ya watu.

Si vyema kuvaa gauni ambalo linabana sana hadi kuonyesha umbo lako lote kazini au haipendezi kuvaa gauni pana sana kama dela kazini kwani utaonekana upo rafu.

Gauni simpo lenye mtindo wa solo huvutia mwanadada au mwanamke mwenye umbo lolote lile.

Huvutia zaidi ikinogeshewa na kijimkanada chembamba kama wewe ni mnene na mkanda mpana kama wewe ni mwembamba kwani itaonyesha zaidi umbo lako.

Advertisement

Pia unaweza kujivalia gauni lako ambalo si pana. Kingine tafuta rangi zile ambazo zinamvuto kwani ukivaa gauni yenye rangi iliyopoa sana itakufanya nawe ufifie.

Hivyo basi, tafuta zile rangi za kung’aa kiasi ili kukupa mwonekano mzuri. Kumbuka rangi hizi huvutia machoni.

TUPIAMO

Usisahau viatu vitakavyokufanya uvutie zaidi. Vaa viatu kulingana na mguu wako ulivyo, viatu virefu havimkatai mtu hata siku moja na mwanamke yeyote yule anaweza kuvaa viatu virefu cha msingi kama wewe ni mnene pendelea kuvaa viatu virefu vyenye visigino virefu.

Tafuta urembo kama cheni na hereni ambavyo vitakufanya upendeze zaidi mara uvivaapo.Beba mkoba wa wastani.

Advertisement